Habari za Punde

*TUNDU LISSU, ALIPOTAKA KUZICHAPA KAVU KAVU NA ANNE MALECELA JUZI


Baada ya Bunge kuahirishwa kutokana na Hotuba ya Mr. Sugu, juzi, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema)  Tundu Lissu na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, walinusurika kuchapana makonde hadharani.

Pichani ni wabunge hao wakiamuliwa na wabunge wenzao wakati wakionyehana ubabe na kukaribia kutoana macho.

Aidha imeelezwa kuwa mtafaruku huo uliibuka baada ya Kilango, kusikika akimtuhumu Lissu kwa uchochezi, akisema kwamba Lissu, amekuwa mbunge pekee anayeongoza kwa vurugu, ambapo maneno hayo hayakumfurahisha Lissu ambaye alishindwa kuvumilia na kumgeukia Kilango kwa nguvu huku baadhi ya wabunge wakishuhudia na wengine wakimzuia Lissu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.