Mwenyekiti wa Mbio za Mbuzi za Hisani Dar es Salaam, Karen Stanley (katikati) akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi yam bio hizo zinazotarajiwa kutimua mbuzi jijini humo Juni 1 mwaka huu katika Viwanja vya The Green, Barabara ya Kenyatta jijini humo. Wengine ni wawakilishi wa baadhi ya wadhamini wa mbio hizo.
************************************************
‘Mbuzi Mmoja tu Anaweza
Kuleta Mabadiliko’
May 23, 2013
Hadi sasa ni mashirika ya
hisani tisa yameshachaguliwa ili yanufaike kutokana na fedha zitakuzopatikana
katika mbio hizo mwaka huu zitakazo saidia kliniki inayowafuata wahitaji waliko
(mobile health clinic), basi kwa watoto wenye ulemavu, kompyuta kwa yatima na
mafunzo kwa wanawake walemavu ya kutengeneza urembo.
Waandaaji wanatumaini
kusaidia vituo na mashirika zaidi ya hisani, lakini hilo litawezekana kutokana
tu na idadi ya watu watakaohudhuria tukio hilo la Juni Mosi mwaka huu, na kiwango
cha fedha kitakachokusanywa siku hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi, Karen Stanley alisema: “Fedha zitakazopatikana ni za muhimu sana
katika kudumu kwa mashirika madogo madogo ya hisani yanayohangaika kutafuta
fedha za kutosha kwa ajili ya miradi muhimu.
“Mwaka jana tuliweka rekodi
kwa kukusanya Shilingi 115 milioni, shukrani kwa wahudhuriaji 4,200
waliolipia getini. Kiasi hiki kilitosha kuongeza idadi ya wanufaika kufikia
mashirika ya hisani 15.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka
2001, mbio hizi za hisani za kila mwaka zimekwisha kusanya zaidi ya Shilingi
660 milioni kwa ajili ya mashirika 60 ya hisani madogo madogo.
Mbio za mwaka huu pia zitatoa
vifaa vya kitaalamu kwa ajili ya watoto waliozaliwa na mtindio wa ubongo, pampu
za maji na matenki kwa yatima na wanawake masikini na pia kwa mradi wa vijana
wa Ukimwi. (tazama orodha ya mashirika hayo chini.)
Mama Stanley alisema: “Kila
mwaka tunajaribu kadri tuwezavyo kuhakikisha kuwa fedha tunazozikusanya kupitia
mbio hizi zinagawanywa kwa vikundi vinavyostahili.
“Huku uhisani likiwa ndio
lengo letu kuu, tusingefanikiwa bila kuungwa mkono na wadhamini wa mbio hizi
Southern Sun, Coca-Cola, Tanzanian Breweries Limited, Mantra Tanzania, Erolink,
FNB na Symbion. Ni lazima pia tuzipeleke shukrani zetu kwa kampuni ya ndege ya
SWISS kwa kutoa tiketi mbili za ndege kwa ajili ya bahati nasibu.
Mbio za Hisani za Mbuzi
zitafanyika Juni 1 eneo la The Green Mtaa wa Kenyatta, kuanzia saa sita mchana
hadi saa 11.30 jioni. Gharama ya tiketi ni Shilingi 5,000 kwa kila mtu wa umri
wowote na zitauzwa getini. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu; www.goatraces.com
No comments:
Post a Comment