Habari za Punde

*WOSIA WA JAY DEE KWA WATANZANIA NIKIFA, KUSAGA NA RUGE WASINIZIKE, CLOUDS WASIPIGE NYIMBO ZANGU


MSANII mahiri wa kike wa miondoko ya Bongo Flava nchini, Judith Wambura 'Lady Jay Dee', ametoa wosia wake kwa aliotaka Waatanzania wote kuuzingatia kabla ya kifo chake.

Katika Wosia huo Jay Dee, amesema kuwa pindi atakapofariki yeye hatokuwa na uwezo tena wa kufungua mdomo na kusema na kuwafukuza 'wabaya' wake kutosogelea kaburi lake ama kujishughulisha na msiba wake.

Wosia wake umekigusa Kituo cha Redio na Tv cha Clouds kuwa hatopenda kituo hicho kutangaza msiba wake pindi atakapofariki wala, Viongozi wa kituo hicho aliowataja kwa majina, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba hatopenda wasogelee Jeneza lake wala kufika katika msiba wake ikiwa ni pamoja na kushiriki kumzika.

Aidha amesema kuwa hatopenda Kituo cha Clouds Fm kupiga nyimbo zake wala kutangaza habari za msiba wake.
''Natambua Kituo hicho kinaweza kutumia redio na Tv yao kutangaza sana kifo changu na kusema Marehemu alikuwa mtu mzuri, mtu wa watu na mengine mengi, na kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi hadi jioni na pengine wakijipendekeza kuuteka msiba wangu na kusimamia mazishi yangu.

Ninachoweza kusema ni kwamba, siku nikifa CLOUDS FM, isipige nyimbo zangu wala isiongelee lolote kuhusu kifo changu, Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga, wasihudhurie msiba wangu na nawaomba watanzania wote mkiwaona watu hawa katika shughuli za msiba wangu, muwapige mawe''. alisema Jay Dee

''Hivi mtu akiwa hawezi kutambua mchango wako wala kukujali ukiwa hai wakati ukiwa na njaa, atajifanya rafiki wa kweli baada ya kufa atakuwa amekusaidia nini kama si majungu tu''. alihoji Jay Dee

Pamoja na wosia huo mkali wa msanii huyo kwa watanzania, lakini bado hakuweza kuweka wazi sababu zilizomfanya kutoa wosia huo utakaocha maswali mengi vichwani mwa watanzania na mashabiki wake kwa ujumla.

Mbali na hayo Jay Dee pia, amejipanga kualika mashabiki 800 katika shoo yake ya uzinduzi wa albam yake ya sita, inayokwenda kwa jina la 'Nothing But The Truth'.

Uzinduzi huo pia utafanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 13 ya tangu alipoanza shughuli za kimuziki, ambapo bonge hilo la Party litafanyika Mei 31 katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, uliopo maeneo ya Namanga jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.