Habari za Punde

*MSANII WA BONGO MOVIE 'KASHI' AFARIKI DUNIA LEO MCHANA

HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa msanii wa filamu nchini Jaji Khamis almaaruf kwa jina la 'Kashi' aliyewahi kutamba katika michezo ya kuigiza katika kituo cha Televisheni cha ITV miaka ya nyuma, amefariki dunia leo mchana katika hosptali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa. 

Akizungumzia kifo hicho cha msanii, Rais wa Shirikisho la wasanii Tanzania, amesema kuwa tasnia yake bado inaendelea kukumbwa na majanga kwa kuondokewa na wasanii ambapo kwa kipindi kifupi wamefariki wasanii kadhaa.
Naye mzee Masinde, ambaye aliwahi kushiriki na marehemu katika michezo ya Luninga, wakiwa kundi moja akiwa kama kiongozi wake, amesema Kashi ni msanii ambaye alikuwa mpiganaji na kwa hakika ni pigo kubwa kwa Tasnia ya Filam kwa kuondokewa na msanii huyo. Mungu ailaze roho ya marehemu Jaji Khamis (Kashi) mahali pema pepponi Amini

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.