Baada ya kutemwa na Klabu yake ya Simba na timu kadhaa kumtolea nje, aliyekuwa kipa namba moja wa Klabu ya Simba, Juma Kaseja, ambaye kwa sasa ni Kipa Namba moja wa timu ya Taifa Taifa Stars, sasa kipa huyo anatakiwa na Timu ya Lipuli ya Iringa iliyopanda Daraja hivi karibuni.
Akizungumza na Kipindi cha Redio One, Katibu wa Klabu hiyo, alisema kuwa baada ya timu hiyo kupanda Daraja imejiwekea mikakati mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kupata Kocha mzoefu na mwenye uwezo, jambo ambalo tayari limekwisha tekelezwa kwa kumpata aliyekuwa Beki wa timu ya Taifa na timu ya Yanga ya Dar es Salaam, Shadrack Nsajigwa, aliyekubali kukinoa kikosi hicho.
Aidha Katibu huyo, alisema kuwa kutokana na maandalizi ya kikosi chao kinachojiandaa na Ligi, ili kufanikisha kupanda daraja na kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom mwakani, iwapo itafanya vizuri ndiyo maana wamejadiliana na kuona kuna umuhimu wa kuandaa fungu maalum kwa ajili ya kumnasa Kipa huyo ili kuisadia timu yao kupanda Daraja.
''Tupo tayari kwa dau lolote kumsajili Juma Kaseja, ili atusaidie kuipandisha timu yetu, na kwa sababu Ligi yenyewe itakuwa ni ya mkataba wa miezi mitatu, tutakuwa tayari kumuachia iwapo atahitaji kuondoka kwenda kujiunga na timu yeyote itakayomhitaji kwa wakati wowote'', alisema Katibu huyo.
Juma Kseja, baada ya kutemwa na Simba, alielezwa kutakiwa na Klabu ya Azam Fc, lakini baadaye viongozi wa Klabu hiyo, walisikika kukana kutomhitaji kipa huyo kwa kile walichodai kuwa wanamakipa walioimara na bado wanamsaada mkubwa kwao, baada ya hapo alizushiwa kutua Klabu ya Coastal Union ya Tanga, ambako nako viongozi wa Klabu hiyo nao wakaruka kimanga na baadaye akazushiwa kutua Mtibwa Sugar, nako akakanwa futi mia na Sasa anahitajika Lipuli ya Iringa, je atakubali kutua kwa dau lolote kuipandisha daraja timu hiyo?

No comments:
Post a Comment