Mwenyekiti wa Sekretariati ya Jukwaa
la Maendeleo Mkoa wa Rukwa
Bw.Joachim Sikulumbwe kushoto ,akiongea na
waandishi wa habari kuhusu mkakati wa kuanzisha chuo kikuu katika mkoa
wa Rukwa kulia ni Mjumbe wa Sekretariati
JUMARU Bw.Titus Simsamba.(picha na Lorietha Laurence-Maelezo)
Jennifer Chamila-Maelezo
MKOA wa Rukwa unatarajia kuanzisha chuo kikuu ambacho kitasaidia vijana wengi wanaokosa
nafasi za kuendelea na elimu ya juu kwa kupata
nafasi ya kujiunga na chuo kikuu.
Mkakati huo unaosimamiwa
na Jukwaa la Maendeleo Mkoa wa
Rukwa(JUMARU) ambao ni halali chini ya sheria za nchi ilioanzishwa mwaka 2009
na wakazi wa mkoa wa Rukwa(Wanarukwa) kwa lengo la kuunganisha nguvu za wanarukwa
wote ili kuleta maendeleo katika mkoa
huo na wakazi wake.
Akiongea na waandishi
wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Sekretariati wa JUMARU
Bw.Joachim Sikulumbwe amesema kuwa wameandaa kongamano la wanarukwa wote
waishio jijini Dar es Salaam litakalo fanyika Septemba 01 mwaka huu,katika ukumbi wa Ubungo –Urafiki Social
hall.
“Kongamano hilo
litazungumzia maliasili na
rasilimali za mkoa wa Rukwa na maendelao
yake ,kiuchumi,kisiasa,kijamii na kiutamaduni nawaomba wanarukwa wajitokeze na
kuhudhuria kwa wingi”alisema bw. Sikulumbwe,
Naye Makamo mwenyekiti
kamati ya wahadhiri mchakato wa chuo kikuu
cha Rukwa bw.Bernard Kasimila amesema sababu ya kuanzisha chuo hicho ni
kuwezesha vijana wenye sifa za kuendelea na masomo kupata fursa ya kujiunga na
chuo kikuu.
Mkoa wa Rukwa ni
sehemu ya Tanzania iliyoko nyanda za juu kusini
yenye wakazi zaidi ya milioni moja kwa sense ya 2012 , una wilaya
3, halmashauri 4,tarafa 17,kata 64,na vijiji 202,unajishughuli zaidi
na kilimo,uvuvi na utalii.

No comments:
Post a Comment