Habari za Punde

*WIZARA YA HABARI YATILIANA SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA IYF

Mandhari ya ukumbi wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo kulikofanyika hafla  ya utiaji wa saini ya mikataba ya ushirikiano  leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo 
Bibi Sihaba Nkinga (kulia) akibadilishana hati  za makubaliano ya 
mikataba ya ushirikiano na Mwanzilishi wa  kikundi  cha  kimataifa cha Vijana kutoka Korea (IYF) Mchungaji Mwandamizi Ock Soo Park (kushoto) leo  jijini Dar es Salaam. Mchungaji Mwandamizi huyo ambaye ametia saini 
kwa niaba ya  kikundi cha IYF (International Youth Fellowship).
 Hafla hiyo pia ilishuhudiwa na  Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na 
Michezo Dkt. Fenella Mukangara (katikati).
Mkurugenzi wa Idara ya  Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, 
Utamaduni na Michezo,Dkt, Elisante Ole Gabriel (kulia)akiongea katika 
hafla ya kutiliana saini mikataba ya ushirikiano leo jijini Dar es Salaam
 baina ya Wizara yake na Kikundi cha Kimataifa cha Vijana 
kutoka Korea (IYF).
Pichani  aliekaa katikati ya bendera ni Waziri wa Habari, Vijana, 
Utamaduni naMichezo  Mh,Dkt. Fenella  Mukangara.( kulia aliokaa) 
Ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bibi Sihaba Nkinga. (kushoto)
 Mwanzilishi wa IYF , Mchungaji Mwandamizi Ock Soo Park kutoka 
kanisa la Good News Gangnam. Seoul Korea.
Baadhi ya vijana wa kikundi cha IYF kutoka korea wakiohudhuria katika 
hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo. Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akipokea Tuzo kutoka kwa Mwanzilishi wa  IYF ya Korea Ock Soo Park ,  ambaye pia ni Mchungaji Mwandamizi wa Kanisa la Good News 
Gangnam. Dhumuni ya tuzo hiyo ni kwaajili yakumpongeza  Mh,Waziri  huyo kwa jitihada za kazi zake.
Waziri akishukuru kwa kupewa Tuzo.
Picha ya Pamoja.
************************************
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo imetiliana saini Mikataba  ya Ushirikiano na Kikundi cha Kimataifa cha Vijana cha ‘International Youth Fellowship (IYF)’ cha Korea.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Sihaba Nkinga ametia saini  Mikataba hiyo kwa niaba ya Wizara wakati Mwanzilishi wa IYF Mchungaji Ock Soo Park ambaye pia ni Mchungaji Mwandamizi wa kanisa la Good News Gangnam  la nchini Korea ametia saini kwa niaba ya IYF.

Utiaji saini huo ulishuhudiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara.
Pamoja na utiaji saini wa mikataba hiyo ya Ushirikiano, Mchungaji Ock Soo Park pia alitoa tuzo ya kuthamini mchango wa kazi azifanyazo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara.

Akizungumza baada ya utiwaji huo wa saini, Dkt. Fenella alitoa shukrani zake za dhati kwa Kikundi cha IYF kwa kazi nzuri  wanazozifanya za kutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana wa kitanzania ambayo yanawawezesha vijana wengi kubadilika fikra zao kutoka hasi kuwa chanya.Pia alimshukuru Mchungaji Ock Soo kwa tuzo aliyompatia.

Kikundi cha vijana cha IYF kimekuwa kikiendesha kambi zake nyingi hapa nchini  ambazo zinaandaliwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kauli mbiu ya kambi hizo kwa mwaka huu ni “Badilisha Fikra kutoka mtazomo hasi kuwa chanya”

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.