Makamu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza
matembezi ya mshikamano wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya
kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni
Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni.
Makamu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza
matembezi ya mshikamano wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya
kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni
Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni.
Makamu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi
Kadi mmoja kati ya wanachama wapya 159, Semeni Sudi, waliojiunga na CCM, wakati wa sherehe za
Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi
Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni. Wanachama hao wamejiunga na CCM
katika kipindi cha maandalizi wa sherhe hizo na kufikisha idadi ya wanachama
wapya 1259 waliojiunga katika kipindi hicho.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi ya kuku Moshi Mlaponi, aliyeibuka kidedea katika shindao la
kufukuza kuku wakati wa Bonanza la michezo ya kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa
CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi jana jioni.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi
zawadi ya Mbuzi kwa wachezaji wa timu ya Makatibu Wenezi wa CCM Wilaya ya
Temeke, walioshinda katika mchezo wa Soka dhidi yao na Wenyeviti wa CCM Wilaya
ya Temeke katka Bonanza la michezo ya kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa CCM,
zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi jana jioni. Timu hiyo ilishinda
bao 1-0.
Wachezaji
wa timu ya Makatibu Wenezi wa CCM Wilaya ya Temeke, wakishangilia ushindi wao
huku wakiwa wamebeba Mbuzi wao juu baada ya kukabidhiwa na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa sherehe za
Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi
Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni.
Baadhi ya Wanachama wa CCM, wakicheza muziki kwa furaha wakati wa sherehe
hizo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwahutubia wananchi wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa
CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya
Temeke, jijini Dar es Salaam, jana
jioni.
************************************************
MAKAMU WA RAIS
AWAASA WANA-CCM DAR ES SALAAM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameongoza wana-CCM wa mkoa wa
Dar es salaam katika sherehe za kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM
zilizofanyika jana kote nchini.
Katika sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja
vya Kituo cha Mabasi Kibada maeneo ya Kigamboni Dkt. Bilal aliwataka wana-CCM
nchini kuendelea kujenga imani na chama chao kwa kuwa kimeongoza kwa miaka 37
kwa amani na utulivu na kuleta maendeleo makubwa kwa wananchi.
Makamu wa Rais ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati
Kuu ya CCM alisema pamoja na changamoto zinazojitokeza Chama hicho kimeendelea
kudumisha amani na kuimarisha demokrasia nchini.
“Tunakerana…lakini hatukamatani mashati,
hatupigani mapanga. Wako wachache wanaandamana lakini CCM kimetulia na
kuendelea kudumisha amani na utulivu,” alisema Dkt. Bilal. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Akizungumzia kuhusu Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar, Makamu wa Rais aliwaambia wananchi hao kuwa muungano wa serikali
mbili unapaswa kuendelezwa kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili za
muungano.
Akijibu malalamiko ya wananchi wa Kigamboni
kuhusu kuchelewa kutolewa kwa fidia ya nyumba zao kufuatia mpango wa serikali
wa kujenga mji wa kisasa wa Kigamboni Dkt. Bilal alisema atamwagiza Waziri wa
Ardhi na Maendeleo ya Makazi akutane na wananchi hao na kuwajulisha hatua
iliyofikia katika kuwalipa fidia zao.
Makamu wa Rais ambaye pia ni mlezi wa CCM mkoa
wa Dar es salaam, alisema mpango wa kujenga mji wa kisasa wa Kigamboni ni mradi
mkubwa ambao utatekelezwa na serikali na kusisitiza ni muhimu wananchi
washirikishwe hatua kwa hatua katika suala zima la kuwapatia fidia zao.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
3/2/2014A
Meza
Kuu, ikitafakari....
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimpongeza msanii wa mashahiri, Abdallah Nyang’anyi, baada ya kughani
mashahiri yake wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM,
zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya
Temeke, jijini Dar es Salaam, jana
jioni.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akishangilia na kumpongeza James Silas, baada ya kujiunga na CCM akitokea CHADEMA,
wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye
Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es
Salaam, jana jioni. Kushoto ni
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza
Abdallah Nguru, akijitambulisha baada ya kujiunga na CCM akitokea CUF, wakati wa
sherehe za Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja
wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Meza
kuu ikishiriki kula kiapo na wanachama wapya waliokabidhiwa kadi zao katika sherehe
hizo jana.
Baadhi ya Wanachama wapya waliokabidhiwa kadi zao katika sherehe hizo jana.
Makamu akiondoka kwenye Uwanja huo baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.















No comments:
Post a Comment