Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WA UWAKILISHI JIMBO LA KIEMBESAMAKI LEO.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitumbukiza  kura yake ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, wakati wa uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo, uliofanyika leo asubuhi mjini Zanzibar. . Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Kituo chake cha kupigia Kura, kwa ajili ya kushiriki kupiga kura ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki katika uchaguzi mdogo, uliofanyika leo mjini Zanzibar leo asubuhi. Kushoto ni Mgombea wa Jimbo hilo, Mahmoud Thabit Kombo. Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita .
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimchagua kwa siri mgombea wa Jimbo la Kiembesamaki, katika uchaguzi mdogo wa Mwakilishi wa Jimbo hilo, uliofanyika leo mjini Zanzibar. Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita.
 Baadhi ya Wananchi wakisoma ubao wa matangazo kutafuta eneo walilopangiwa kupigia kura ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, wakati wa zoezi hilo lililofanyika leo asubuhi mjini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.