
MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya wenyeji Yanga na Mbeya City iliyochezwa jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza jumla ya sh. 175,285,000.
Mechi hiyo iliyokuwa na ushindai mkubwa kutokana na 'Wabishi' Mbeya City kutofungwa katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo, ulihudhuriwa na jumla ya watazamaji 30,411 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Na mwisho wa mchezo huo Yanga ndiyo iliibuka na ushindi wa bao 1-0, na kufanikiwa kuvunja mwiko wa timu hiyo kutofungwa.
Mgawanyo wa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 26,738,389.83, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,919,200 wakati kila klabu ilipata sh. 42,960,086.50.
Uwanja sh. 21,844,111.53, gharama za mechi sh. 13,106,466.92, Bodi ya Ligi sh. 13,106,466.92, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 6,553,233.46 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,096,959.36.
Nayo mechi ya Simba na Oljoro JKT iliyochezwa Februari 1 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 47,705,000 ambapo kila timu imepata sh. 11,254,122 kutokana na watazamaji 8,267.
Mgawanyo mwingine katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Simba kushinda mabao 4-0 ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 7,277,033.90 na gharama za kuchapa tiketi sh. 2,278,400.
Uwanja sh. 5,722,434.92, gharama za mechi sh. 3,433,460.95, Bodi ya Ligi sh. 3,433,460.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,716,730.47 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,335,234.81.

No comments:
Post a Comment