Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas
Kashililah akitoa maelezo juu ya kazi mbalimbali zifanywazo na Bunge la Jamhuri
la Muungano wa Tanzania leo wakati wa sherehe fupi ya utiaji saini mkataba
wathamani ya dola laki moja za kimarekani kati ya Chama cha Kupunguza matumizi
ya silaha na Maridhiano cha China na Ofisi za Bunge la Jamhuri la Muungano wa
Tanzania.
Baadhi ya viongozi toka pande zote mbili wakiwa katika
sherehe ya utiaji saini mkataba wa thamani ya dola laki moja za kimarekani
kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya ofisi za Bunge la Jamhuri la Muungano wa
Tanzania uliofanyika leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas
Kashililah (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi
ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association
for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan wakitia saini mkataba huo wa
thamani za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo
jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas
Kashililah (kulia) akimkabidhi zawadi mgeni wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha
kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese
Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan (kushoto) mara
baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano wenye thamani za fedha za
kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es
Salaam.
Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas
Kashililah (kulia) akiwakabidhi zawadi baadhi ya wajumbe alokuja nao mgeni
wake.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha
na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for
Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan (kushoto) akimkabidhi zawadi Katibu wa
Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (kulia) mara baada
ya utiaji saini mkataba wa makubaliano wenye thamani za fedha za kimarekani
dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas
Kashililah (aliyekaa kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na
mgeni wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na
Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace
and Disarmament) Bi. Chen Huaifan (aliyekaa mstari wa mbele kushoto) mara baada
ya utiaji saini mkataba wa makubaliano wenye thamani za fedha za kimarekani
dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.
China na Tanzania
zatiliana saini mkataba wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani.
Na. Benedict
Liwenga-MAELEZO.
16/05/2014
OFISI ndogo ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania leo
imetialiana saini na Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha
Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and
Disarmament) wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani.
Utaiji saini huo umefanyika leo katika Ofisi ndogo za Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukihusisha viongozi wa pande zote mbili
akiwemo Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas
Kashililah pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya
Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association
for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas
Kashililah amesema kuwa mkataba huo wenye thamani ya dola laki moja za
kimarekani utasaidia ofisi ya Bunge kuweza kupata vifaa mbalimbali vya ofisi
vikiwemo kompyuta, mashine ya kudurufu, vipaza sauti, kamera pamoja na vifaa
vya kurekodia.
“Ndugu zetu kutoka China pamoja na hiki Chama chao wamesaini
pamoja nasi mkataba wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani ambao
wametutaka sisi tuamue wenyewe ni vifaa gani tunahitaji kwaajili ya ofisi yetu
ya Bunge mjini Dodoma ili wao waweze kutununulia na kutukabidhi”. Alisema
Kashililah.
China na Tanzania zimekuwa zikitiliana saini mikataba
mbalimbali ya maendeleo ambayo kwa namna moja mikataba hiyo imekuwa
ikizinufaisha pande zote mbili kiuchumi na mpaka hivi sasa uhusiano huu umedumu
kwa muda miaka hamsini.










No comments:
Post a Comment