Menu

Saturday, May 17, 2014

*HAWA NDIYO WANAOONGEZA KINA KIREFU CHA MTO MBEZI ENEO LA BONDE LA KAWE, WAHUSIKA MPO???

 Pamoja na kupigwa marufuku mara kadhaa wachimabji hawa bado wameendelea kuchimba mchanga katika Mto Mbezi huku wakijaza magari makubwa yasiyo na idadi na tena wakifanya kazi hii mchana kweupe bila hata kuwa na woga. Wachimbaji hawa wamekuwa wakifanya hivi kila inaponyesha mvua kubwa inayokusanya mchanga mwingi kutoka eneo jingine kusogeza eneo hili, lakini wao wamekuwa wakiuhamisha mchanga huo kwa kuuchimba na kuupakia katika magari na kisha kwenda kuuzwa. Je asubuhi mpaka jioni ni kweli hakuna mhusika hata mmoja anayepita eneo hili na kuona jambo hili, au wachimbaji hawa ni wa wahusika???? kwa siku za nyuma iligundulika kuwa magari yaliyokuwa yakipakia mchanga eneo hili yalikuwa ni mmoja kati ya kigogo mwenye mamlaka katika kusimamia hili kutoka Kata hiyo.
 Wachimbaji wakiendelea na kazi...
Wahusika hamuwaoni hawa??????

No comments:

Post a Comment