Habari za Punde

*KOCHA PLUIJM ATIMKA YANGA, SASA KUTUA KUIFUNDISHA SHOALA FC YA SAUDI ARABIA

Kocha Hans van Der Pluijm wa Yanga anaondoka leo kwenda Saudi Arabia kusaini mkataba mpya.

Kocha huyo anakwenda kuingia mkataba na timu ya Ligi Kuu ya Shoala FC ambayo imevutiwa na kazi yake.


Pluijm amepata timu ya kuifundisha nchini Saudi Arabia.
Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu Pluijm amesema kuwa ameamua kuipa kisogo YAnga baada ya kupata ofa kubwa kutoka kwa Klabu hiyo ya Saudi Arabia.

“Ofa ni kubwa sana, yoyote asingevumilia kuiacha na nimezungumza na viongozi wa Yanga, wamekubaliana na uamuzi wangu.

“Natarajia kuondoka kwenda Saudi Arabia, baada ya kusaini mkataba nitarudi hapa na kuisaidia Yanga kupata wachezaji,” alisema.

Pluijm ameinoa Yanga kwa nusu msimu na kuiwezesha kushika nafasi ya pili.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.