Menu

Friday, May 23, 2014

*MALAWI WATUMIA BARUA PEPE NA VIPEPERUSHI KUHESABU KURA, NAIBU WAZIRI SERIKALI MITAA MALAWI AJIUA KWA RISASI

 Maafisa wa uchaguzi nchini Malawi, wanasema kuwa wamelazimika kutumia vipepesi na barua pepe kujumlisha kura za uchaguzi mkuu baada ya mfumo wa elektroniki kuharibika.
Makarani wa tume ya uchaguzi waliopo mashinani wameshindwa kutuma tarakimu za matokeo ya kura hizo.

Haya ndio matatizo ya hivi punde kushuhudiwa katika uchaguzi huo lakini maafisa wamesema wamejitolea kufanya kazi.

Katika baadhi ya maeneo masanduku ya kura hayakuwasilishwa na baadhi ya vituo vilichelewa kufunguliwa siku ya jumanne na kulazimisha maafisa kutumia ndoo na katarasi za plastiki kukusanya kura.

Rais wa sasa Joyce Banda, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wagombea wengine 11. Kutokana na baadi ya vituo vilifungua kuchelewa Jumanne na kusababisha shughuli ya upigaji kura kuongezwa muda kwa siku ya pili.

Uchaguzi wa Malawi ulikumbwa na visa vingi vya wizi wa kura pamoja na udukuzi wa mitambo iliyokuwa inatumiwa kujumlisha kura. Haya ni madai ya Rais Joyce Banda.
Rais Joyce Banda ametaka kura hizo kuhesabiwa upya bila ya kutumia mitambo ya elektroniki ya kuhesabu kura.
Bi Banda alikumbwa na ushindani mkali katika uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumanne kutoka kwa wagombea watatu akiwemo, waziri wa zamani wa mambo ya nje Peter Mutharika.
*NAIBU WAZIRI SERIKALI MITAA MALAWI AJIUA RISASI
Wakati yakijiri hayo naye Waziri Naibu Waziri wa Serikali za mitaa wa Malawi, Sajiu, mapema usiku wa kuamkia leo ijumaa alijipiga risasi na kujiua akiwa nyumbani kwake mjini Lilongwe.

Godfrey Kamanya alikuwa anagombea kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Nzonzi Kusini.
Alijiua alfajiri ya kuamkia leo katika mojawapo ya vyumba vya nyumba yake iliyopo Area 10 mjini Lilongwe.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali kuu ya Kamuzu mjini humo, na jeshi la polisi litatoa taarifa rasmi ya kifo hicho baada kukamilisha uchunguzi.

Haijajulikana sababu za Kamanya kujiua japokuwa ameacha barua ya maelezo ambayo polisi wataitoa baadae. Matokeo ya kura bado hayajatangazwa rasmi katika kile kinachosemekana kuwa uchaguzi wenye ushindani mkali sana.

No comments:

Post a Comment