Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete iliyoko Kijitonyama wakimsikiliza kwa makini Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ndiye mlezi wa shule hiyo wakati alipoitembelea leo mchana.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiangalia ngoma ya asili iliyokuwa ikichezwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Salma Kikwete iliyoko Kijitonyama katika Wilaya ya Kinondoni. Mama Salma aliitembelea shule hiyo leo
Afisaelimu wa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Omath Sanga akisoma taarifa ya elimu ya wilaya kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati Mama Salma alipoitembelea Shule ya Sekondari Salma Kikwete iliyoko Kijitonyama
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Salma Kikwete wakati alipoitembelea shule hiyo
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Kinondoni wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Ndugu Jordan Rugimbana (kulia kwa Mama Salma ) na walimu na wafanyakazi wa Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete
No comments:
Post a Comment