Mh.Saada M.Salum
akifafanua jambo katika moja ya Mikutano ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) na watendaji wa mashirika mbalimbali ya Kimataifa,Kulia kwa
Mh.Waziri ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha – Dkt. Servacius Likwelile na Kushoto
ni Bwa.Peter Noni Mkurugenzi Mkuu wa
Benki ya Rasimali Tanzania (TIB).
Mh.Waziri wa Fedha
Saada Mkuya Salum na Washiriki mbalimbali wa Mkutano wa mwaka wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano huo uliofunguliwa na
Mh.Paul Kagame katika ukumbi wa Mount Karisimbi Jijini Kigali Rwanda.
**********************************************
Serikali ya Tanzania ipo imara katika
kuendelea na kusimamia juhudi zinazofanywa na Banki ya Afrika katika kuinua
mitaji kupitia mpango wa sita wa kukuza mitaji wa benki hiyo (GCI-VI).
Mh.Saada amesema kuwa kupitia mpango wa GCI-VI Tanzania imekuwa na uwezo wa kulipa hisa zake
zipatazo Dola za Kimarekani 2,683,429.52 katika awamu ya tatu kwa muda
uliopangwa.
Saada amesema kuwa kupitia mpango wa GCI-VI
Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kulipa hisa zake zipatazo Dola za
Kimarekani 2,683,429.52 katika awamu ya tatu kwa muda uliopangwa.
Zaidi ya hayo, Waziri Saada
ameendelea kusema kuwa nchi yake imeweza kulipa hisa zake za awamu ya nne
zipatazo kiasi cha Dola za Kimareka 1,279.30 kabala ya muda uliopangwa.
“Ninaamini ni katika mkutano huu
tunaweza kujadili dira ya Benki katika miaka mingine 50 ijayo kama kauli mbiu
ya mkutano huu inavyothibitisha, “Afrika tunayoitaka miaka 50 ijayo” alisema
Waziri Saada.
Aidha, Waziri Saada alimpongeza
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Donald Kaberuka na uongozi mzima kwa kusimamia
na kuongoza kwa umahiri mkubwa majukumu walionayo ya kibenki na kuhakikisha
inasonga mbele daima na kuifanya kuwa benki bora barani humu.
Ili kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa bara hili lazima
kudumisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kijamii na kujipatia
maendeleo endelevu kwa nchi zao na watu wake. Mwaka
huu Benki ya Afrika inafikisha miaka 50 tangu kuasisiwa kwake ambapo imeendelea
kuhudumia bara hili kwa mafanikio makubwa.
Kwa upande wake Rais wa Rwanda Paul Kagame akifungua mkutano
huo alisema kuwa ili kufikia uchumi wa kati katika Bara la Afrika kwa miaka 50 ijayo inabidi nguvu kubwa ielekezwe kwenye
sekta binafsi ambayo itatengeneza ajira kwa vijana na wanawake.
Mkutano huo ni wa siku
tano kuanzia 19 hadi 23 Mei mwaka huu ambapo kabla ya ufunguzi wa Mkutano huu
ulitanguliwa na mikutano mbalimbali ya Magavana ambao ni Mawaziri wa Fedha
kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakiambatana na wajumbe kuwakilisha nchi
zao.


No comments:
Post a Comment