Habari za Punde

*KARIBU KATIKA BLOG MPYA YA UJENZI ZONE

Habari Mdau, Pole na kazi za kujenga Taifa, Nilikuwa naomba msaada wako wa kunitambulishia Blog ambayo nimeianzisha kwa sababu ya Ujenzi, kusaidiana maswala mbalimbali yanayohusu ujenzi nina ambatatinisha kila kitu hapa chini.
Asante sana
Jackqueline 
**************************************
Karibuni wadau wote  katika Blog yenu  mpya ya wanaujenzi, hapa tutakuwa pamoja  kushirikiana kwa mawazo, ushauri,  ujuzi tulioupata wenyewe na kwa ujuzi wa wataalamu waliosomea fani ya ujenzi. Kama wewe unajenga nyumba yako mwenyewe, kama umewahi kujenga, kama unajipanga kujenga na hata kama una ndoto kwamba siku moja utajenga nyumba,  Basi karibu sana katika blog Hii kujua mengi.

Toa mchango wako wa mawazo, tujulishe umefanikiwa vipi kutatua matatizo uliyokabiliana nayo kwenye ujenzi, wako mshauri mwenzio ambae anatafuta njia ya kufanikisha azma yake na anatamani nae akae kwenye nyumba yake mwenyewe, uliza swali kwa jambo linalokutatiza au toa ushauri kuhusu kitu chochote unachoona unaweza kuchangia na wanaujenzi tukanufaika nacho, hakuna mtu mmoja anayejua kila kitu, ila kwa kushirikiana pamoja tunaweza.

Familia ya wanaujenzi inamjumuisha kila mmoja wetu, iwe umejenga ghorofa, iwe umejenga chumba kimoja, iwe ndiyo kwanza unajinyima ili ukanunue kiwanja, hapa ni mahala pako.

Mwisho
Changamoto ni nyingi kwenye safari ya ujenzi wa makazi yetu, tupo hapa kuelimishana, kupeana moyo na zaidi kurahisisha zoezi zima la ujenzi, kushirikiana uzoefu ndio hasa lengo la Blog hii ya Ujenzi Zone. Chochote kinachohusu ujenz kwa mtazamo chanya kitafaniakisha zaidi lengo la Blog hili kutimia.

TEMBELEA SASA BOFTYA HAPA : www.ujenzizone.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.