Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepete, Luiza Mbutu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mchcna huu, wakati akiwatambulisha wanamuziki waliokuwa viongozi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki (kushoto) na Super Nyamwela (wa pili kulia) waliojiunga na bendi hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka
**************************************
MWANAMUZIKI mahiri wa muziki wa dansi nchini na kiongozi wake wa Show, mahiri, Super Nyamwela, leo wametangazwa rasmi kurejea kundini kujiunga na bendi yao ya zamani ya African Stars Twanga Pepeta, baada ya kuipa kisogo bendi hiyo siku za nyuma na kusimamia iliyokuwa bendi ya Extra Bongo.
Wanamuziki hao walikuwa ni miongoni mwa wanamuziki waliounda kundi zima la Twanga Pepeta siku za nyuma kabla ya kujiengua na kujiajiri katika bendi yao ya Extra Bongo.
Choki na Nyamwela walivunja bendi yao ya Extra Bongo na kutangaza kuifungwa kwa muda usiojulikana na wao kutimkia nchini Japan, ambako walikwenda kupiga shoo kadhaa kwa mwaliko wa mwanamuziki mkongwe Mtanzania anayeishi nchini humo, Fresh Jumbe.
Baada ya kumaliza maonyesho kadhaa waliyokuwa wameandaliwa nchini Japan, wanamuziki hao walirejea nchini wiki iliyopita huku zikivuma tetesi kuwa tayari ilishakamilika mipango ya kujiunga na bendi yao ya zamani.
Akiongea na Mtandao huu wa Sufianimafoto, Super Nyamwela, mara baada tu ya kutua nchini, alisema kuwa shoo zao nchini Japan zilikwenda vizuri na zilikuwa na mwitikio jambo ambalo limewapatia mialiko mingine kadhaa inayotarajia kufanyika miezi kdhaa ijayo.
Alipoulizwa kuhusu kujiunga na Twanga Pepeta, Nyamwela, alisema kuwa bado hawajapata taarifa rasmi za kutakiwa kujiunga na bendi hiyo, na kuongeza kuwa iwapo wataitwa na bosi wao wa zamani basi watakuwa tayari ila kwa kuangalia zaidi maslahi kabla ya makubaliano.
''Kinachotakiwa zaidi ni kuangalia maslahi, kwani toka tuna siku ya pili leo toka turejee nchini lakini hatujasikia lolote kutoka kwa Bosi wetu wa zamani na kama atatuhitaji sisi tupo tayari,
Bendi yetu ya Extra Bongo tuliifunga kutokana na safari yetu ya ghafla lakini nahisi kama hatutaweza kuirejesha kwa kipindi kifupi hiki kutokana na tatizo la usimamizi na hasa kwa upande wa pesa ikiwa ni pamoja na miishahara ya wafanyakazi, ujue kuendesha bendi inabidi uwe kamili''. alisema Nyamwela
Na leo yametimia yale yaliyokuwa yakisemwa wakati wanamuziki hao wakiwa nchini Japan, kuwa wakirejea tu nchini Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta, ameshaaandalia kitita cha kuwarejesha kundini ili kuimarisha bendi yake, jambo ambalo limefanyika leo.
Na kwa upande wa Choki, alisema kuwa, amerejea Twanga Pepeta bila shinikizo la mtu yeyote na kwa sasa hana mpango wa kuhama tena bendi hiyo.
"Mimi nimeamua mwenyewe kwa akili zangu timamu kurejea kundini Twanga Pepeta na wala sijashawishiwa na mtu yeyote, na hivi sasa sina mpango wa kuihama tena bendi hii, na tayari nimeshaandaa jumla ya nyimbo tatu kwa ajili ya mashabiki wangu wa Twanga Pepeta, ambazo ni “Kichwa Chini”, “Usiyaogope Maisha” na “No Discussion” ''. alisema Choki
Aida imeelezwa kuwa bendi hiyo iko mbioni kuwarejesha wanamuziki wake wote walioihama kama Victor Mkambi, ambaye mazungumzo bado yanaendelea ambapo aliazimwa kupiga kinanda siku ya mpambano wa Nani mkali kati ya Twanga na Fm Academi, uliofanyika mwishoni mwa wezi uliopita, pamoja na Charls Baba, ambaye pia anasubiriwa amalize mkataba wake katika bendi ya Mashujaa.
Wanamuziki hao wamepangiwa Onyesho la kwanza la utambulisho wa kurejea kundini, ambalo litafanyika tarehe 18 katika ukumbi utakaotangazwa hapo baadae.

No comments:
Post a Comment