Mwenyekiti
Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Abraham Mengi, akimvisha pete ya ndoa Miss Tanzania mwaka 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe
‘K-Lynn’ wakati wa ibada yao ya ndoa.
Mengi akiwa na furaha na mkewe K-Lynn baada ya kufungishwa ndoa.
Dkt. Mengi na mkewe, wakikata keki.....
Maharusi
na wapampe wao wakitembea ufukweni sambamba na watoto wao mapacha.
Maharusi wakipiga picha ya pamoja. Wa pili kushoto ni Nancy Sumari (Miss
Tanzania na Miss World Africa 2005) na mumewe Luca.

MISS Tanzania mwaka 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe ameacha
historia ya aina yake nchini, baada ya kufunga ndoa na Mwenyekiti Mtendaji wa
makampuni ya IPP, Dk. Reginald Abraham Mengi, tukio lililofanyika nchini
Mauritius mwishoni mwa mwezi uliopita.
Jack,
ambaye pia anafahamika kwa jina lake la kisanii kama K- Lynn, anaacha historia
hiyo nchini Tanzania kwani licha ya kufunga ndoa hiyo akiwa tayari na watoto
wawili mapacha aliozaa na mumewe, pia ndiye mshindi wa kwanza wa shindano hilo
kubwa, kuolewa na bilionea baada ya kuwa katika uhusiano kwa miaka kadhaa
pasipokuwa na kashfa na miezi minne baada ya kuvalishwa rasmi pete ya uchumba.
K-Lynn
ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, anaweka pia historia hiyo kwa
kuolewa na mmoja wa wafanyabiashara wakubwa na wenye kuheshimika katika Afrika
Mashariki, ambaye licha ya kumiliki vyombo vikubwa vya habari vikiwemo redio,
magazeti na televisheni, pia ni mmiliki wa viwanda, migodi ya madini na
biashara nyinginezo kubwa. IPP inamiliki vituo vya Radio One, Capital Radio,
East Africa Radio, ITV, Eatv, Capital TV na magazeti la Nipashe, The Guardian
na mengine kadhaa.
Harusi yao
inayotajwa kuwa ni moja kati ya ndoa za kifahari nchini Tanzania, ilihudhuriwa
na idadi ndogo ya watu wapatao 50, ambao ni ndugu wa karibu wa familia hizo
mbili, pamoja na marafiki muhimu wa pande zote mbili.
Mengi,
anayetajwa kuwa tajiri wa tatu nchini, miezi minne iliyopita, alimvalisha pete
ya mchumba msanii huyo aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kufanya muziki, wakati wa
sherehe ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika jijini Dar es
Salaam na kuhudhuriwa pia na watu wachache.
Baadhi ya
washindi wengine wa shindano la Miss Tanzania walioolewa ni pamoja na Hoyce
Temu (1999), Miriam Magese (2001) Faraja Kota (2004), Nancy Sumari (2005) na
Sarah Israel (2011).





No comments:
Post a Comment