Basi la Air Jordan lenye namba za usajili T650 AQZ, linalofanya safari zake Mwanza-Dar es Salaa, lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea jijini Dar, likiwa limeanguka ubavu baada ya kupata ajali eneo la Migua Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora mchana huu na kuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Emmanuel (aliyekandamizwa na basi hilo hapo chini) na kujeruhi jumla ya watu 20.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzan Kagama, alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi uliomshinda dereva wa basi hilo kwenye kona na kutereza na kisha kuingia pembezoni mwa barabara na kuanguka. Aidha kamanda Suzan alisema kuwa majeruhi hao wamepelekwa kupatiwa matibabu katika Hospitali ya wilaya ya Nzega, na kuongeza kuwa tayari basi hilo limeshainuliwa kwa juhudi za wananchi wa eneo hilo.
Baada ya ajali hiyo ya leo wadau wamehoji kulikoni ajali hizo kuendelea kutokea kila kukicha na kwa kipindi cha muda mfupi ambapo tayari Taifa limeshapoteza idadi kubwa ya wananchi wake, ambapo siku za nyuma ilizoeleka ajali nyingi kutokea kipindi cha mwisho wa mwaka, kulikoni safari hii ni mfululizo tena mwanzoni mwa mwaka?? na kuongeza kuwa huenda Ugaidi umeingia nchini kwa njia hii ya ajali za kila kukicha?
Majeruhi wakiwa eneo la ajali....
Majeruhi wakipatiwa huduma ya kwanza eneo la ajali hiyo.
Majerhi wa ajali hiyo wakipatiwa huduma ya kwanza.....
Baadhi ya abiria walionusurika na wananchi wa eneo hilo wakiwa eneo la ajali.
Raia wakiwa eneo la ajali hiyo. Picha kwa Hisani ya Mdau Nzega







Jamani hii ni ushirikina kutokana na uchaguzi mkuu wanatafuta roho za watu. Sio bure
ReplyDelete