Habari za Punde

*HAFLA YA UTOAJI WA NISHANI ZA KUMBUKUMBU YA MIAKA 50 YA MUUNGANO VIWANJA VYA IKULU DAR

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Tanzania wakisimama wakati wimbo wa taifa ukipigwa baada ya kumalizika hafla ya sherehe ya utoaji wa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili,Tatu na Nne jana katika viwanja vya Ikulu Jijini Dares Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika sherehe za utoaji wa nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano wa madaraja mbali mbali  katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam jana.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha  Jaji Mkuu Msataafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha  Bw.Mabrouk Jabu Makame Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Bw.Damian Zefrini Lubuva baada ya kumvalisha  Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam katika kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha nishani Bw.Aboud Talib Aboud wakati wa hafla ya kutunuku Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu katika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha  Cpl Laura Philip Mushi  Nishani ya Ushupavu wakati wa utoaji wa Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Madaraja mbali mbali katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilali pamoja na Viongozi wengine wakiwa  katika picha ya pamoja baada ya kumalizika hafla ya sherehe ya utoaji wa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili,Tatu na Nne jana katika viwanja vya Ikulu Jijini Dares Salaam.
 Miongoni mwa Wananchi na Viongozi walioteuliwa kutunikiwa nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano wa madaraja mbali mbali wakiwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya kutunikiwa nishani zao.
Miongoni mwa Viongozi na Wananchi  walioteuliwa kutunikiwa nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano wa madaraja mbali mbali wakiwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya kutunikiwa nishani zao ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar jana. Picha na Ikulu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.