Habari za Punde

*MAVETERANS WA BARCELONA WAWAFUNGA MAVETERANS WA TANZANIA 2-1

 Nahodha wa timu ya Maveterans wa Barcelona, Patrick Kluivet, akiingia uwanjani huku akiwa amembeba mtoto wenye ulemavu wa ngozi, 'Albino' wakati wamchezo wa kirafiki kati yao na Tanzania Stars Veterans, uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Katika mchezo huo Barcelona walishinda mabao 2-1.
 Mchezo huo uliingia dosari baada ya mchezo kuchelewa kuanza huku mashabiki wakipiga kelele kulalamikia muda na pia waandaaji walipoamua kuwaruhusu mashabiki wa mzunguko kuhamia nafasi za VIP ili kujaza eneo hilo kutokana na kutokuwepo na watu katika eneo hilo jambo lililoelezwa na wengi kuwa lilichangiwa na kiwango kikubwa na kiingilio kilichotangazwa, ambapo baadaye ilitangazwa kuwa kiingilio kikubwa zaidi ilikuwa ni Sh. 100,000 badala ya 300,000 kama ilivyokuwa ikitangazwa.
 Akijiandaa kupiga krosi.
 Juma Kaseja akiwania mpira na Patrick Kluivert
 Mustapher Hoza (kulia) akiwania mpira na mchezaji wa Barcelona.
 Kaseja akiokoa hatari langoni kwake
Hoza akiutoa mpira wa hatari mbele ya adui..KWA PICHA ZA MATUKIO KIBAO YA MTANANGE HUU ZITAKJIA BAADAYE, KAA NASI

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.