Habari za Punde

*MECHI YA YANGA, ETOILE YAINGIZA SH. MIL 223

Mchezo no.91 wa Kombe la Shirkisho barani Afrika (CC) hatua ya 16 bora uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam, kati ya wenyeji timu ya Young Africans dhidi ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia umeingiza jumla ya sh. 223,135,000.
 Jumla ya watazamaji 36,105 walikata tiketi kuhudhuria mchezo huo, huku VIP A zikikatwa tiketi 68, VIP B tiketi  869, VIP C tiketi 582, Orange tiketi 1,955 na viti vya rangi ya Bluu na Kijani tiketi 32,631 ziliuzwa.
Mgawanyo wa mapato ni VAT 18% sh. 34,037,542.37, Gharama ya tiketi sh. 11,462,000, Gharama ya Uwanja 15% sh. 26,645,318.64, Gharama za mchezo 15% sh. 26.645,318.64, CAF 5% sh. 8,881,772.88, TFF 5% sh. 8,881,772.88 na Young Africans 60% sh. 106,581,274.58.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.