Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles
Kitwanga, akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini, uliofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam, ulioanza jana na kumalizika leo. Mkutano huo una lengo la kujadili mafanikio na changamoto
katika utendaji kazi wa Wizara
pamoja na taasisi zake.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara
ya Nishati na Madini wakifuatilia
kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Charles Kitwanga (pichani juu).
Sekretarieti inayoratibu
mkutano wa baraza la wafanyakazi
la Wizara ya Nishati na Madini wakisikiliza kwa makini na kunukuu
mada zilizokuwa zinawasilishwa katika mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa
Wizara ya Nishati na Madini wakiimba
wimbo wa kuonyesha mshikamano ujulikanao kwa jina la “solidarity
forever”
Baadhi
ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi
kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwasilishwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE) Wizara ya Nishati na Madini, Marcelina Mshumbusi, akisoma hotuba ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi
Mwihava (pichani chini) katika mkutano
huo. Kushoto ni Katibu wa TUGHE Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi
Mwihava (kulia) akisoma hotuba ya
kumkaribisha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga
(wa kwanza kushoto). Katikati ni Katibu wa TUGHE Wizara ya Nishati na Madini,
Assa Mwakilembe.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga
(kushoto) akisalimiana na Mhasibu Mkuu Mfawidhi wa Wizara ya Nishati na Madini, Michael Marandu (kulia)
mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano ili kufungua mkutano huo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles
Kitwanga (katikati, waliokaa mbele) na
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava ( wa pili kutoka kushoto, waliokaa mbele)
wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi, Wizara ya Nishati na Madini. Picha na Miraji Msala wa Sufianimafoto.com
No comments:
Post a Comment