Habari za Punde

*PICHA ZA MTANANGE WA YANGA v/s MBEYA CITY UWANJA WA TAIFA DAR JANA

 Mrisho Khalfan Ngassa, akiwekwa mtu kati na beki pamoja na kipa wa Mbeya City, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga ilishinda mabao 3-1.
 Mrisho Ngassa, akienda hewani kupiga mpira wa kichwa.
 Ngassa, akijiandaa kumiliki mpira mbele ya beki wa Mbeya City.
 Kpah Sherman, akichuana kuwania mpira na beki wa Mbeya City, Juma Nyoso..
 Sherman, akipasua msitu wa mabeki wa Mbeya City.....

Sherman, akiifungia timu yake bao la kwanza....
 Amis Tambwe, akimchachafya beki wa Mbeya City.....
 Bado Tambwe, akimfinya beki wa Mbeya City....
 Bado Tambwe, akimtoka beki wa Mbeya City....
 Simon Msuva, akimramba chenga beki wa Mbeya City.....
 Mzee wa chenga za maudhi, Haruna Niyonzima, akimchekecha beki wa Mbeya City....
 Niyonzima akimfinya beki wa Mbeya City....
 Niyonzima akiondoka zake baada ya kumchekecha beki huyo.....
Mashabiki wa Yanga, wakishangilia ushindi wa timu yao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.