Habari za Punde

*RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AWASHA MWENGE WA UHURU MKOANI RUVUMA LEO

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwasha mwenge wa Uhuru Kitaifa katika uwanja wa Majimaji Songea Mkoa wa Ruvuma leo(kushoto) Waziri wa Vijana Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara na Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa jamii vijana wanawwake na watoto Bi Zainab Mohammed.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge kwa mwaka 2015 Juma Khatibu Chum(kushoto) akimkabidhi  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kulia)  Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Songea Profesa Norman Sigalla King(kulia) Mwenge wa Uhuru uhuru kwa ajili ya kuanza mbio wilayani humo baada ya uzinduzi ulifanywa leo mjini Songea  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa  Juma Khatib Chum baada ya kuuwasha leo katika uwanja wa Majimaji Songea Mkoa wa Ruvuma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani Ruvuma. Picha na Frank Shija na Tiganya Vincent, Songea

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.