Habari za Punde

*YANGA YAJIPIGIA MBEYA CITY, NJIA YA UBINGWA NYEUPEEEE

 Mshambiliaji wa Yanga, Amis Tambwe, akimtoka beki wa Mbeya City, Juma Nyoso, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga ilishinda mabao 3-1, yaliyofungwa na Kpah Sherma katika dakika ya 18, Salum Telela dakika ya 38 na Nadir Haroub 'Canavaro' dakika ya 49.  Bao la Mbeya City, lilifungwa na Themi Felix katika dakika ya 39. Kwa matokeo hayo sasa Yanga imefikisha jumla ya Pointi 46, Azam Fc wakiwa na Pointi 37.

Dakika ya 53 Themi Felix, alizawadiwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu, Salum Telela aliyeshindwa kuendelea na mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Mrisho Ngassa.
 Kipa wa Mbeya City, Hanington Kalyesubula, akiruka kudaka mpira wa hatari langoni kwake.
 Simon Msuva, akimwegemea beki wa Mbeya City na kupiga shuti lililombabatiza beki wa Mbeya City na kutoka nje.
Bonge la kabari, si Kung fu bali ni soka. KWA MATUKIO ZAIDI YA PICHA ZA MTANANGE HUU ZITWAJIA BAADAYE, KAA NASI.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.