TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Kufuatia mgogoro wa kisiasa, jaribio la kumtoa madarakani Raisi wa Jamhuri ya Burundi, Pierre Nkurunziza na maelfu ya wananchi wa nchi hiyo kukimbilia nchi jirani za
Tanzania na Rwanda.
Hali ya kambi zinazopokea wakimbizi zinaonekana kuelemewa na kupelekea kuhatarisha hali za wakimbizi hao.
Kutokana na hali hiyo, Bunge
la
Afrika ya Mashariki kupitia kamati yake ya Masuala ya Jumuiya na Usuluhishi wa Migogoro imeteua wajumbe watakao kwenda kutembelea kambi hizi zilizopo Kigoma-Tanzania
na Mashariki mwa nchi ya Rwanda kwa madhumuni yafuatayo;
1.
Kujiridhisha na hali ya mazingira ya kambi hizo na kuangalia mipango ya kutatua mgogoro huo.
2.
Kuangalianakutimizajukumu la Bunge la
Afrika Mashariki kupata suluhisho la kudumu la mgogoro ulioko sasa nchini Burundi.
3.
Kuwatemebelea na kuwafariji wananchi wote wa
Burundi walioko kwenye kambi hizo.
Wajumbe wa kamati teule wamegawanyika katika makundi mawili,
wajumbe watakaokwenda Kigoma-Tanzania wataongozwa naMhe. Abdullah
Mwinyi ambae ni mwenyekiti wa kamati hiyo na wajumbe watakaokwenda Mashariki mwa Rwanda
wataongozwa naMhe. AbubakarZein.
Imetolewana;
Mhe. Abdullah Mwinyi
No comments:
Post a Comment