Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara aliofanya katika viwanja vya Ofisi ya CCM, wilaya ya Sengerema mjini, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Mwanza, jana.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano wa Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ofisi ya CCM, wilaya ya Sengerema mjini, jana.
Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, akieleza alivyoshiriki katika utekelezaji wa ilani ya CCM, alipohutubia mkutano wa katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM wilaya ya Sengerema mjini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo wakati wa mkutano wake wa hadhara uliofanyika jana, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM wilaya ya Sengerema mjini. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwasili kuhutubia mkutano wa hadhara aliofanya katika Viwanja vya CCM, wilaya ya Sengerema mjini, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Mwanza, jana.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimhoji Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja kujua imekuwaje hadi hali ya soko kuwa mbaya, alipokagua vyoo na kushuhudia hali mbaya, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza, jana.
Kwa hiyo mradi huu ndiyo umekwamia palee, siyo", Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimuuliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Mathew Lubongeja, alipokagua mradi wa Kilimo cha Skimu, Katunguru, alipokagua mradi huo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama, katika Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza.
Mradi huo ambao ni mkubwa umekwama kumalizika kwa madai ya kukosa fedha baada ya kutumia sh. milioni 700 tu, kati ya Shilingi Bilioni 2 zilizokuwa zimekadiriwa kumaliza mradi huo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, fedha hizo zinatakiwa kutolewa na serikali.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa kwenye Kivuko cha Sumar III, alipozindua kivuko hicho kinachoendeshwa na mwekezaji, kwenye eneo la Kamanga, leo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama wilayani Sengerema mkoani Mwanza. Kivuko hicho kinaunganisha Sengerema na Mwanza mjini
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi tangi na chujio la maji la mradi wa maji wa Sengerema mjini uliopo eneo la Nyamazugowa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza, jana
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua ujenzi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Sengerema, jana.
,Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiendesha Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM, Wilaya ya Sengerema, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa chama katika wilaya hiyo mkoani Mwanza, jana.











No comments:
Post a Comment