Habari za Punde

*MKWASA , AULA ARITHI MIKOBA YA BOSI WAKE NOOIJ, KULIPWA MILIONI 25 KWA MWEZI

 Kocha msaidizi wa timu ya Taifa 'Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa, anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari kesho kuhusu uteuzi wake wa kukaimu nafasi ya Kocha Mkuu mkuu wa Stars, huku akirithi, mshahara ule ule wa sh. milioni 25, gari na nyumba.
 Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij, aiwa na huzuni wakati akiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo,alipokuwa akitangazwa rasmi, msaidizi wake kurithi mikoba yake.
**************************************
AKIZUNGUMZA na waandhishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo mchana, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi amesema kwamba, kocha mpya wa timu ya taifa, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa, atakuwa analipwa kiasi cha fedha kama alichokuwa akilipwa kocha Mholanzi, Mart Nooij aliyetupiwa virago juzi.
Nooij aliyekuwa analipwa dola za Kimarekani 12,500 (zaidi ya Sh. Milioni 25) kwa mwezi, alifukuzwa mwishoni mwa wiki baada ya Taifa Stars kufungwa mabao 3-0 na Uganda Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo, Dar es Salaam, Malinzi amemtangaza rasmi Mkwasa kuwa kocha mpya wa Taifa Stars akisaidiwa na kocha Hemed Morocco.

Mkwasa ambaye ni Kocha Msaidizi wa Yanga na Morocco kocha wa Mafunzo watafanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya kuwania kufuzu kwa CHAN na AFCON.

Malinzi amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa timu ya Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana kutoka mashiriksho mengine duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo makocha  hao wazawa wamekizi.

“Kocha Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi  (zikiwemo posho) alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao wazawa” aliongeza Malinzi”


Aidha Kamati ya utendaji ya TFF Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa timu ya Taifa, lengo la uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya kamati ya Utendaji na timu ya Taifa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.