Habari za Punde

*WLF WAENDELEA KUKABIDHI NYUMBA ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA KIJIJI CHA MABANDA WILAYANI KIBONDO MKOANI KIGOMA

 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibondo Ayubu Sebabili (kulia) akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Nyumba ya Mganga yenye uwezo wa Kukaliwa na Familia Mbili baada ya kukabidhiwa Nyumba hiyo na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la World Lung Foundation Dk.Nguke Mwakatundu (wa pili kulia)
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la World Lung Foundation Dk.Nguke Mwakatundu(aliyesimama) akizungumza katika hafla ya kukabidhi Nyumba ya Mganga kwa Uongozi wa Kijiji cha Mabamba Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.
.Katibu Tawala wa wilaya ya Kibondo Ayubu Sebabili (aliyesimama) Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Nyumba ya Mganga kwa ajili ya Watumishi wa kituo cha Afya Mabamba Wilayani Kibondo iliyojengwa kwa Hisani ya Shirika la World Lung Foundation.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la World Lung Foundation Dk.Nguke Mwakatundu (kati kati mwenye suti na tai) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Afya Wilaya ya Kibondo muda Mfupi baada ya kukabidhi Nyumba ya Watumishi wa Afya kwa ajili ya Kituo cha Afya mabamba iliyojengwa kwa Hisani ya Shirika la World Lung Foundation (wa tano kushoto mstari wa mbele) Katibu Tawala wa wilaya ya Kibondo Ayubu Sebabili.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.