Habari za Punde

*BONDIA LULU KAYAGE AIBUKA KIDEDEA AFRIKA YA KUSINI, AMCHAPA MPINZANI WAKE KWA T.K.O

 Yassin Abdallah 'Ostadh' akimwinua juu mkono baada ya kushinda kwa T.K.O raundi ya pili.
 Mwamuzi wa pambano la ngumi la wanawake kati ya Lulu Kayage wa Tanzania (mwenye bluu) na Lizbeth Sivhaga wa Afrika Kusini, akisubiri kumtangaza Lulu kuwa mshindi wa pambano hilo baada ya kumshinda mpinzani wake kwa T.K.O katika raundi ya pili. Kushoto ni Yassini Abdallah 
Bondia Lulu Kayage akiwashukuru mashabiki wawaliokuwa wakimshangilia baada ya kutangazwa mshindi wa pambano hilo, lililochezwamwishoni mwa wiki huko nchini Afrika ya Kusini.

Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' akimwinua mkono juu bondia Lulu Kayage baada ya kuibuka mshindi
*************************************************

BONDIA wa Kike Lulu Kayage mwishoni mwa wiki aliIbuka kidedea nchini Afrika ya kusini baada ya kumdunda vibaya kwa T.K.O mpinzani wake Lizbeth Sivhaga wa nchini hum0.

Bondia huyo ameonyesha uwezo mkubwa katika pambano lake la kwanza la nje ya nchi na kufanikiwa kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili mchezo.

Lulu alianza mchezo huo kwa kasi na kumshambuliwa mpinzani wake bila kumpa pumzi wala mwanya wa kujibu mapigo, huku mpinzani wake pia akionyesha uwezo na kujaribu kutaka kumaliza pambano katika raundi za awali.
 Lulu Kayage, alifanikiwa kumpeleka chini mpinzani wake huyo katika raundi ya pili baada ya kumwelemea  kwa makonde mfululizo na wasaidizi wake kumuokoa kwa kumtupia taulo hivyo kusababisha Lulu kushinda T.K.O ya raundi ya pili
bondia huyo anatarajia kurejea nchini kesho Agost 11 kwa ajili ya maandalizi ya mapambano yake mengine ya kimataifa.

Katika safari hiyo Bondia Ramadhani Shauri amepoteza mpambano wake kwa kupigwa K.O ya raundi ya nne na bondia mzoefu Philip Ndlovu wa Afrika ya Kusini, ambapo mpambano uho wa raundi nane ulijikuta ukisha katika raundi ya nne

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.