Menu

Wednesday, August 19, 2015

*DEREVA WA DALADALA AVUNJA SHERIA MCHANA KWEUPEEEE, APIGWA TANCHI NA RAIA

 Gari la abiria Daladala linalofanya safari zake Makumbusho Posta, lenye namba za usajili T376 CVH, likiwa limezuiliwa na raia mwema ambaye haikuweza kufahamika mara moja ni nani, baada ya kuvunja sheria za usalama Barabarani na kupita njia isiyoruhusiwa katika mzunguko wa Askari Monment Samora Posta mpya. Gari hilo lilitakiwa kuzunguka mzunguko huo na badala yake likakatisha katika njia kulia kwake ili kuliwahi daladala jenzie na kukutana na magari na watu hawa waliolizuia na kulirudisha kuzunguka katika utaratibu wa kawaida.
 Dereva huyo akibanwa na Raia hawa wawili waliokuwa wakimtaka kurudi nyuma na kupita katika utaratibu wa kawaida.
Ama kweli madereva wa daladal wa akili nyingi kuzidi 'matope', eti hapa alikuwa akibishana na raia hawa bila hata kuwajua wakati tayari alikwisha vunja sheria na endapo angekamatwa na askari angelipa faini. 

No comments:

Post a Comment