Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Wa Anga Tanzania (TCAA) Varrely Chanmlunga akimkaribisha Meneja Mipango wa Kimataifa wa Idara ya Uongozaji wa Ndege wa Marekani (FAA) Michele Cappelle wakati wa Warsha ya uongozaji wa ndege barani afrika iliyoandaliwa na Idara ya Anga ya Marekani .Washa hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Uongozaji wa Ndege ya Marekani (FAA) Tony Ferrante.
Baadhi ya washiriki wa Warsha ya uongozaji wa Ndege Barani Afrika iliyoandaliwa na Idara ya Anga ya Marekani (FAA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)leo jijini Dar es Salaam wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa katika warsha hiyo.
Kushoto, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya hudumu toka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA ,Viola Masaku na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uongozaji ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Said Onga wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa warsha ya uongozaji wa ndege barani Afrika iliyoandaliwa na Idara ya Anga ya Marekani (FAA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Uongozaji wa Ndege nchini Marekani (FAA) Tony Ferrante akitoa mafunzo ya uongozaji wa ndege wakati wa warsha iliyowashirikisha waoungozaji ndege kutoka barani afrika ,wakati wa warsha iliyoandaliwa na Idara ya uongozaji wa Ndege ya Marekani na TCAA jijini, Dar es Salaam. Wanao msikiliza kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Wa Anga Tanzania (TCAA) Varrely Chanmlunga, Meneja Mipango wa Kimataifa wa Idara ya uongozaji wa Ndege wa Marekani (FAA) Michele Cappelle na mtaalamu wa mipango wa idara ya uongozaji wa ndege wa Marekani FAA,Rebecca Barther
Washiriki wa warsha ya uongozaji wa ndege barani afrika wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na Idara ya uongozaji wa ndege ya Marekani FAA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA,iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment