Menu

Monday, August 10, 2015

*KIMBISA AMKARIBISHA RAIS KIKWETE MJINI DODOMA

 Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vitakavyofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma.
Ndugu kimbisa alikanusha uvumi uliosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa ameihama CCM. Kushoto ni Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Picha na Freddy Maro
Rais Kikwte, akisalimiana na Abdulrahman Kinana baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuongoza vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vitakavyofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma. Picha na Fredy Maro

No comments:

Post a Comment