Kufuatia tetesi mbalimbali kuhusu ujio wa mkali wa
miondoko ya R&B na Pop NE-YO katika
onyesho la Coke Studio Afrika msimu wa tatu, sasa imethibitishwa kuwa msanii
huyo atakuja rasmi.
NE-YO ambaye atakuwa ndiye mgeni pekee kutoka nje ya Afrika,
ataambatana na nyota wengine wa Afrika ambao ni Wangechi (Kenya), Alikiba (Tanzania), Maurice Kirya (Uganda), Dama Do
Bling (Mozambique) na Ice Prince (Nigeria) ambapo wataungana kufanya nyimbo
moja. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Kuelekea ujio wake nchini Kenya, NE-YO ametoa taarifa rasmi ambayo inasema, “ Ni
heshima kubwa sana kwangu kurejea Afrika na kushirikiana na wasanii kutoka bara
hili, kupitia Coke Studio Afrika, hii ni fursa nzuri inayojenga uhusiano mzuri
miongoni mwa watu wa rangi , makabila na dini zote kujumuika kwa pamoja katika
onyesho hili la kukumbukwa.. Nimefurahi sana kupata wasaa huu wa kujumuika na
wasanii na wanamuziki hawa wenye vipaji vikubwa kabisa.
Mwezi uliopita alitumbuiza katika tuzo za MTV Music ambazo
zilifanyika nchini Afrika Kusini. Akiwa nchini Kenya NE-YO ataungana na nyota watano kutoka nchini za
Kenya, Nigeria, Tanzani, Uganda na Msumbiji kufanya wimbo wa pamoja kwa ajili
ya msimu mpya. Hata hivyo wasanii hao wote kutoka katika nchi hizo wameshafanya
wimbo wa pamoja.
Ndani ya miaka 10, NE-YO ametoa albamu sita. Albamu yake ya
kwanza kabisa ni My Own Words was a bona fide R&B game changer bearing
classics: “Stay”, “So Sick”, “When You’re Mad” and “Sexy Love”. Albamu yake ya
hivi karibuni ya Non–Fiction, iliachiwa mwezi Januari mwaka huu. Albamu hiyo
ilishika nafasi ya tano nchini Marekani miongoni mwa albamu 200 bora, na
kumfanya NE-YO kuwa mwanamuziki wa kiume wa pili kuwa na albamu 6 mfululizo
zilizoingia kumi bora.
NE-YO amefanikiwa kujikusanyia tuzo mbalimbali ulimwenguni
na kuwa miongoni mwa watunzi mahiri wa nyimbo zinazotikisha ulimwenguni,
ikiwemo ile aliyoshirikiana na Rihana ya “Unfaithful” and Beyonce’s
“Irreplaceable”. Hivi karibuni NE=YO ametangazwa kujiunga na moja vipindi
maarufu vya ‘series’ za runinga cha ‘Empire’ kama mtunzi wa mziki, msimu wa
pili wa ‘Empire’ unatarajiwa kuanza mwezi Septemba.
katika Coke Studio
Afrika msimu wa 2 mwaka jana,
mwanamuziki Wyclef Jean alitumbuiza wimbo wake uliokuwa ukitikisa wa “Divine
Sorrow”, akipewa ushirikiano wa karibu na wasanii wengine wakiwemo Rabbit,
Chidinma na Shaa.
Mpaka sasa katika msimu huu wa tatu, imeshuhudiwa wanamuziki
kama Chameleone, Olamide, Jua Cali, Elani, Vanessa Mdee, 2 Face Idibia, Fid Q,
Juliana Kanyamozi na Neyma na wengine wakiwa tayari wamesharekodi wimbo wao wa
pamoja
Muwania tuzo ya Grammy, ambaye ni mwanamuziki na muandaaji
pia Zwai Bala kutoka kundi la TKZee maarufu kwa mziki wa Kwaito nchini Afrika
Kusini, amekuwa ndio muongozaji huku Brett Lotriet, muongozaji na muandaaji maarufu
wa kimataifa wa runinga atakuwa ndiye muandaaji wa mlolongo wa matukio
yanayorekodiwa.
Lengo kuu la Coke Studio Afrika ni kuwakutanisha kwa pamoja
wasanii mbalimbali wa Afrika na kuimba
nyimbo ambazo zina vionjo tofauti hivyo kuongeza msisimuko. Lakini vilevile
kutoa fursa kwa wasanii wachanga
kushirikiana na wakubwa ili kuwapa changamoto ya kuongeza ujuzi katika
kazi zao na kuzidi kukuza vipaji vyao
No comments:
Post a Comment