Menu

Friday, August 14, 2015

*NHIF YATOA MAFUNZO KWA WAMILIKI NA WANAHABARI WA MITANDAO YA KIJAMII, YAJA NA KIKOA

 Mwenyekiti wa Mabloggers Tanzania TBN, Joachim Mushi, akizungumza wakati wa  Mafunzo maalum kwa waandishi wa habari za mitandao, Wamiliki wa mitandao ya Kijamii iliyoandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya NHIF, iliyofanyika jijini Dar es Salaam, jana.
 Mkurungezi Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF, Athumani Rehan,  akifungua mafunzo hayo maalum kwa waadishi wa mitandao ya kijamii (Blogger).
Baadhi ya Wanahabari na Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa  katika mafunzo hayo.
 Mtoa mada, ambaye ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF, Eugen Mkongoti,  akifafanunua baadhi ya mada mbalimbali zilizotolewa wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya waadishi na Wamiliki wa Mitandao ya kijamii   (Bloggers) waliohudhuria mafunzo hayo yaliyoandaliwa na NHIF wakiwa bize kunasa walichokuwa wakifundishwa katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki
Sayed Abdul kutoka blog ya Bagamoyo akitoa neno la shukrani kwa waandaaji wa mafunzo hayo mara baada ya kumalizika.
 Washiriki. Picha na Miraji Msala
*************************************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
Mpango wa Taifa wa Bima ya afya ni shirika la umma lililoaazishishwa kwa Sheria na 8 ya mwaka 1999 ya bunge la Jamhuri ya Tanzania kwa lengo kuweka utaratibu wa upatikanaji wa huduma za afya nchin kwa njia rahisi na kwa uchangia nafuu. 

Makundi yanayohudumiwa na mfuko huu ni kama , watumishi wa serikali kuu,mashirika  ya umma, waajiriwa wa  makampuni binafsi  yaliyojiunga kwa hiari yao,wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ,watumishi  wastaafu,Vikosi vya jeshi la Polis vilivyo chin ya Wizara ya Mambo ya Ndan ya Nchi,Viongozi wataasisi za dini na watu binafsi.

Katika jitahada za kupunguza wigo wahuduma za afya kwa jamii mfuko umekuja na mpango mpya Unaoitwa KIKOA. 

Mpango wa Kikoa ni utaratibu wa utoaji wa huduma ya afya kwa kadi kwa vikund/ushirika ambavyo watu wake wamejiajiri na kupata kipato kwa msimu.

Mfano wafanya biashara ndogo ndogo,Saccos,vikoba,umoja wa watu wa bodaboda, nk Kila mwanachama mmoja anatakiwa kichangia kiasi  sh 78,800 na kujipatia matibabu kwa mwaka mzima.
 MKURUGENZI wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
 MKURUGENZI wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti, akifafanua jambo wakati alipokuwa akiwasilisha mada juu ya mpango wa uchangiaji binafsi, KIKOA, wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NHIF, na Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN).Warsha hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Bloggers wakimsikiliza  Mkurugenzi wa huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti, alipokuwa akiwasisilisha mada iliyohusu mpango wa uchangiaji binafsi, KIKOA kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NHIF na Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN).Warsha hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini jijini Dar es Salaam.
  MKURUGENZI wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti,akiwasilisha mada juu ya mpango wa uchangiaji binafsi, KIKOA, wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NHIF, na Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN).Warsha hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Bloggers wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye Warsha hiyo
 Wadau wakifuatilia jambo
 Bloggers wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye warsha hiyo 
  Baadhi ya Bloggers wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye Warsha hiyo
Blogger Mzee Kitime akichangia jambo katika semina hiyo ya iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NHIF na Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN).Warsha hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment