Habari za Punde

*RAIS KIKWETE AKAGUA BIDHAA ZA KILIMO MAONESHO YA NANE NANE MKOANI LINDI

 Mtaalamu wa Kilimo Dkt.Kissa Kajigili akimpa maelezo ya kilimo bora cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji wa kisasa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipotembelea maonesho ya nane nane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia moja ya matrekta katika viwanja vya maonesho Ngongo Mkoani Lindi wakati wa maadhimisho ya sherehe za wakulima Nanenane.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia muhogo uliolimwa kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo wakati wa maonesho ya kilimo yaliyofanyika katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima yaliyofanyika kitaifa mkoani humo.

Mjasiriamali Bi.Ashura Omary Mswazi akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete mafuta aliyokamua kwa mashine bora na kuyauza kupitia kampuni yake ya Kwadelo Investment wakati Rais alipotembea na kukagua baadhi ya mabanda ya maonesho katika viwanja vya Ngongo Mjini Lindi wakati wa sikukuu ya wakulima nanenane. 
Bonge la Mhogo. Picha na Freddy Maro

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.