Menu

Tuesday, September 1, 2015

*RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI MAKAO MAKUU YA ULINZI LUGALO

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kitambaa wakati wa uwekaji jiwe la msingi la Ujenzi wa National Defence Headquarters huko Lugalo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi  Jenerali Davis Mwamunyange,Watatu Kushoto ni Waziri wa Ulinzi Dkt.Huessein Ali Mwinyi na kulia ni Bwana Hu mwakiklkishi wa kampuni ya ujenzi kutoka China.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akimuonyesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mchoro wa majengo ya Makao Makuu ya Ulinzi yatakayojengwa eneo la Lugalo jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
 Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa National Defence Headquarters huko Lugalo jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ulinzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi muda mfupi baada ya kuwasili eneo la Lugalo kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa National Defence Headquarters
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Makamanda wa Jeshi la Ulinzi wakati wa uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi. Picha na Freddy Maro. 

No comments:

Post a Comment