Menu

Wednesday, August 26, 2015

*SERIKALI YASAINI MKATABA WA ZAIDI YA SH. BILIONI 422 KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NCHINI.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akisaini hati ya makubaliano ya mkopo nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia ili kuimarisha sekta ya afya nchini katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi Bella Bird.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo nafuu na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi Bella Bird (kulia) mara baada ya kusaini hati hiyo ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia ili kuimarisha sekta ya afya nchini leo jijini Dar es salaam. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kuimarisha sekta ya afya nchini leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi Bella Bird.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Deo Mtasiwa (kulia) akisisitiza jambo wakati hafla ya usatiji saini hati ya makubaliano kuimarisha sekta ya afya nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia leo jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya waandishi wa habari na viongozi wa serikali na wawakilishi wa Benki ya Dunia waliohudhuria hafla ya kusaini hati ya makubaliano ya mkopo nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia katika kuimarisha sekta ya afya nchini leo jijini Dar es salaam. Picha Eleuteri Mangi-MAELEZO

No comments:

Post a Comment