Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo, baada ya kukaa kimya kwa kipindi tangu mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho chini ya mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa, alipotangaza rasmi kujinga na chama hicho baada ya kukatwa jina lake katika kinyang'anyiro cha kuwania urais na CCM. Leo ameibuka na kusema ya moyoni kuwa amejivua uanachama rasmi wa chama cha Chadema pamoja na Ukatibu Mkuuu wa Chama hicho na kuaachana kabisa na siasa kutokana na mambo yaliyokuwa yakifanyika ndani ya chama chake ambayo alisema kuwa hayakumlidhisha na hakukubaliana nayo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kupata taswira nzuri za Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya wananchi pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dk. Wilbroard Slaa leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment