Wengi walianza kuvutiwa na neno hill, Mshenga wake ambaye ni Bishop Gwajima alinipigia simu kunijulisha kuwasha kuwa kule Dodoma mambo yamekwishaiva na nini kifuatwe.
Kawaida ukipokea mtu ambaye hajajisafisha mwenyewe kuna hatari kuwa ule uchafu utahamia kwako Kwa sababu hajajisafisasha kwa kiwango kinachotegemewa.
Siwezi kuwa namsafisha mtu kwa sababu siwezi kumsafisha kabla hajajisafisha
mwenyewe huko alikotoka.
Swali langu nililiweka kwa wenzagu tangia mwanzo, kwamba, Lowasa anakuja kama mtaji au anakuja kama mzigo?
Suala sio Urais. Mpaka siku ile sijachukua fomu ya urais. Suala halikuwa Dr Slaa anataka kumzuia Lowasa kugombea Urais!
Safari hii mchakato ukianza mapema tangia mwezi februari.
Urais wangu binafsi hauwezi kuikomboa Tanzania bila ya misingi na vigezo vilivyokamilika!
Na kama ni asset anakuja na nani? Na wafuasi hao ni wa aina gani? Vijana wa bodaboda, vijana wa mtaani wasio na kazi. Vijana waliokumbwa na propaganda au viongozi serious watakaoweza kusaidia kuongoza mapambano!
Wabunge 50, Wenyeviti wa mikoa 28, wenyeviti wa wilaya 88.
Mimi, Mbowe, Gwajima na Tundu Lissu tulibishana kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa tisa jioni. Tukashindwa kukubaliana. Na tukapishana mambo kadhaa.
Niliwaambia kuwa sikanyagi nyumbani kaa mtu. Lowasa ni mwanachama wa CCM. Siwezi kwenda nyumbani kwake kwenda kumpigia magoti
Niliandika barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya ukatibu mkuu nikiwa humohumo ndani ya Kikao. Prof Safari akaichana barua yangu hapo hapo na nikaandika barua nyingine tena hapo hapo na nikwakabidhi tena.
Dr Slaa haya mambo yamepangwa. Usijisumbue. Funga mdomo wako. Hilo ndilo jibu nililopewa ukumbini humo baada ya barua ya pili, Nikaondoka!
Kwa upande wangu mimi huwa naona kuwa, Siasa ni sayansi. Haitaki ulaghai. Haitaki udanganyifu.
Niliandika barua ya kuacha siasa.
Kilichoendelea
Siasa haitaki propaganda kama una nia ya kulikomboa taifa.
Toka saa tatu mpaka saa tisa tupo na Mbowe, Gwajima na Lissu muda wote. Iweje Josephine anizuie?
Sisi katika familia yetu tumezoea propaganda hizo! Kagueni kama kuna jina la Josephine kama amepokea senti moja.
Dr Slaa na watoto wake wameendelea kula muhogo kama tulivyoahidi. Hela zetu zilienda kupigania taifa hili!
Kikubwa katika siasa ni cradability ya chama ulichokijenga lakini pia mwanasiasa makini hawezi kukubali jina lake liharibiwe
Maslahi mapana ya taifa ni lazima yapimwe kwa vigezo vipana na sio unavyoona wewe kwa macho yako na kusikia kwa masikio yako na maslahi yako
Ni seme kwa bahati mbaya wamekuwa waongo kwa sababu hakuna kigezo hata kimoja tulichokiweka na kikatekelezwa, Iweje uje kujiunga na Chadema baada ya kukatwa jina lako CCM kwa kuonekana Kuwa ni mzigo na hufai, Hapo ni dhahiri Umetafuta kichaka cha kujifichia. Umekimbilia mahali.
Wanakuja watu kama Sumaye. Mtu ambaye watanzania wanajua kuwa hata mwenyewe hakuwa safi, yeye mwenyewe ni fisadi.
Kule Bungeni Nilimwita yeye mwenyewe fisadi, kwa sababu alichukua shamba la Magereza kule Kibaigwa. Halafu leo unakuja kusema wewe ni safi na Lowassa ni safi!
Hivi dhambi inahalalishwa kwa dhambi nyingine. Watanzania walimwita Sumaye Mr Zero!
Hawakukosea, kwani Kama mtakumbuka Sumaye huyo huyo akiwa CCM, aliwahi kusema katika mkutano wake na waandishi wa habari, kuwa iwapo CCM watapitisha jina la Lowassa kuwania urais basi yeye ataondoka CCM.
Sasa imekuwaje aondoke CCM baada ya kukatwa na si kupitishwa jina lake na bado kumfuata huko Chadema na kumkumbatia na kumsafisha eti Lowassa ni msafi wakati hata yeye mwenyewe si msafi.
Tunagemea wabunge makini. Mnatuletea makapi. Ni rejects, wakati mimi niliwatangazia watanzania kuwa chadema mwaka huu hatupokei makapi!
Wenyeviti wenyewe waliokuja ni mizigo. Nani hajui Msindai kuwa ni mzigo. Nasubiri ajibu chochote nimuwekee machafu yake hadharani!
Mgeja simjui siwezi kumsemea kitu ila hao wengiene wote ni makapi!
Mara nikasikia anakuja mtu anaitwa Chili, nikauliza Chizi ni nani katika nchi hii. Wakanimabia kuwa sifa ya chizi ni mwizi wa kuiba kura. Kama tunataka kuiba kura ni kwa nini tusimamie sera yetu ya kuupinga ufisadi?
Ukweli daima una upande. Hakuna ukweli
Nani hajui Guninita alivyo reject tangia umoja wa vijana. Alipokuwa chadema nikimtuma kazi anarudi hawezi hata kuandika hata page moja! Siasa ya ulaghai mimi siitaki
Wamefika hatua ya kusema kuwa hata kama ni lazima tuweke mkataba na shetani ili tuiondoe CCM.
UKIWAONDOA wale vijana wanaonufaika barabarani wataweza kupata hafueni
Unaondoa CCM kwa program makini na si longolongo, walikuwa na imani na misingi isiyoyumba. Uadilifu. Leo kuna uadilifu?. Kuna watu wanasema msiwatuhumu watu kama hawajapelekwa Mahakamani, Upuuzi
Lowasa anatufunga mdomo hata tusikemee makosa ya ufisadi unakuwa reasonable doubt na sio absolute doubt, kuna usemi huu, atakayempotosha huyu myoofu anatakiwa afungwe jiwe atupwe baharini na kamwe Dhambi haihalalishwi kwa dhambi nyingine.
CCM hawana ujasiri. Wamekuwa waoga kuchukua hatua kwa watu wanaostahili. Wamelea haya matatizo Kwa muda, Lowasa amefikia hapa kwa sababu ya kulelewa na CCM
TANZANIA tunatamaduni zetu, kama choo, Choo ni mahali pa uchafu. Mtu akipakuwa Choo na kuhamisha chumbani kwake, Chumba chake ndiyo kinakuwa choo. Kwa maana hyo Chadema sasa ni Choo maana imehamisha uchafu kutoka chooni na kuukumbatia tena Chumbani wala si sebuleni.
Haya zungumza na wewe sasa ni choo!
Nilikuwepo bungeni wakati wa suala la Richmond. Kama huyajui funga mdomo au ufungwe jiwe tukutupe baharini uache upotoshaji
Nilimwambia Lowasa acha kulalamika, acha kunung'uka. Sema Richmond ni ya nani? Toka hadharani huyo mkubwa ni nani?
Niligongewa na kuletewa rushwa ya Sh. milioni 500 ili niachane na kusemea suala hili na Richmond. Mimi nalipwa milioni 500 je unazo ngapi? Unapotoa rushwa hiyo kuzuia taarifa kuingia bungeni. Hiyo dhambi ikoje?
Ripoti ikaenda kuibiwa iwekwe hadharani
Kamati ya Mwakyembe ilienda kuomba kibali wapewe taarifa ya baraza la Mawaziri.
Na Suala hili lilianza wakati wa mkapa. Ilipoingia serikali ya Rais Kikwete Cabinet ya 10/2/2006 ilitaka kuendelea na mchakato lakini kufuata taratibu! Kwenye cabinet alikuwepo Lowassa.
Na baada ya mambo kuharibika, Lowasa alikimbia kabla ya bunge kumjadili kwa sababu alijua kuwa litaenda kumfukuza.
Kulikuwa na makampuni 26. Waliorudisha walikuwa kampuni 8. Kamati ya tathmini ilipima na kuona kuwa hakuna anayefaa. Msabaha alielekeza na kufuta mara nne tenda hiyo.
Leo Chadema yangu niliyoshiriki kuijenga nayo imeanza kuleta na kujaza watu uwanjani kwa mabasi. Siko tayari kujuta na kuumia wote kama wote tulikuwa mazezeta. Nakataa kuwa zezeta. Nasimamia misingi yangu!
Ajenda yetu ya kwanza ilikuwa rushwa. Ajenda yetu leo nini? Msingi wa matatizo yetu leo
Leo ajenda hiyo chadema tuna kigugumizi cha kuisema!
Ilani ya CHADEMA haikuandaliwa na Lowassa juzi. Kwa hiyo ni cut and paste. Hakuna jipya la Lowasa!
Sura ya sisi CHADEMA kugeuka kuwa wabovu zaidi ya CCM, LAZIMA muingie usiku kwa sababu mmesafirishwa kutoka mikoani, Watu wenyewe mnaotaka kujenga maadili wote mmehusika na uchafu!
Scotland Yard inaandika kuwa Lowassa achunguzwe kwa paundi milioni 400. Halafu watu wanatokea kutaka kumtetea! Eti kesi yake haikuenda Mahakamani na kama Mwakyembe alisema kuwa kesi ya jinai haina mwisho.
Kazi ya kwanza ni kusafisha uchafu. Kesi ya Richmond ni sehemu ya uchafu. Lowassa ni sehemu kuu ya uchafu huo. Watanzania mnaliwa kwa sababu ya umbumbu na ushabiki
Taifa linaibiwa mabilioni halafu tunaambiwa leteni ushahidi kama hamna shut up. Ni kauliz ya Lowasa. Udikteta! Lowasa ni dikteta!
Sitaku kuingia kwenye mambo ya Babu Seya.
Kama Lowassa akili yake haiko sawa. Nadhani anapaswa kupimwa. Kesi ya Ulawiti Rais hana mamlaka ya kuiondoa! Ataagiza mahakimu na majaji. Uhuru wa mahakama uko wapi?
Kesi ya ugaidi. Waziri Mkuu alikuwa nani? Nani aliagiza mapolisi waingie msikitini na mbwa kwenda kukamata watu. Leo anapiga propaganda kama rafiki wa waislamu!
Rais anayependa kutafuta hisani ya kura kwa kuapili kwa watu ambao hawajui... Huyo Rais ni balaa!
Hitimisho:
Kama taifa tuna kazi kubwa ya kuchambua. Siyo tu shamrashamra na sio tu maneno matamu kwa sababu maneno matamu yametufikisha pabaya.
Unapizubgumza utendaji uliotukuka tuangalie kupima na kutafiti. Msiwe makasuku wa kuripoti nakupngeza yenu. Tumpime Lowasa huko alipofanyia kazi.
Eti ametukuka kwa utendaji. Sumaye mpaka leo hawezi kupita pale mvomero. Alichukua ardhi ya ilipotaka kujengwa makao makuu ya wilaya!
Atoke hadharani kuongelea hisa zake ambazo hajaweka katika fomu zake za maadili!
Ukieleza ukweli ukweli daima utaelekea upande. Truth is one and it is indivisible. Yamewatandika CHADEMA Kwa sababu ndiyo ukweli ulivyo!
Nimestaafu siasa lakini sio kuwa sina nchi. Mimi ni mtanzania. Mtetezi wa watanzania. Na nitabaki!
Nitawatumikia watanzania kwa jinsi mwenyezimungu alivyonipa kipawa!
Sijapata vitisho katika maisha yangu yote kama kipindi hiki. Hata wakati niliposema list ya
Mshenga aliwahi kunitamkia kuwa huyu mbwana anaungwa na watu wote. Kanisa la kilutheri hana shida nalo kwa sabau hili ni kanisa lake. Huo ni udini!
Aliniambia kuwa kati ya maskofu 34 wa katoliki. 30 wamehongwa. Kwa hiyo wote tufuate!
Na pesa zilikuwa zinagawanywa mbele ya macho yangu kati ya kilioni sitini hadi milioni 300
[01/09/2015 19:34] +255 672 223 269: Kutoka Serena Hotel Ambako Dr. Slaa Anaongea
1.Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutujali uzima.
2. Nimeamua kujitokeza leo hii ili kumesha upotoshaji na kuuweka wazi ukweli.
3.Sina tabia ya kuyumbishwa na ninasimamia ninachokiamini.
4.Sina ugomvi na kiongozi yeyote maana siasa sio uadai.
5. Siasa inapoongozwa kwa misingi ya upotoshaji, matokeo yake ni vurugu.
6. Naweka wazi kuwa mimi sikuwa likizo na hakuna aliyenipa likizo yoyote.
7.Kilichotokea ni kuwa niliamua kuachana na siasa tangu 28.7.2015 saa sita usiku baada ya
kutoridhishwa na kilichokuwa kinaendelea ndani ya chama changu.
8.Ni kweli nilishiriki kumleta Lowassa CHADEMA Lakini nilikuwa na misimamo yangu ambayo ilitufanya
tusielewane.
9. Baada ya Lowassa kukatwa pale Dodoma, Gwajima ambaye ni mshenga wa Lowassa alinipigia simu
kutaka kujua nii cha kufanya.
10. Nilimpigia Mwenyekiti Mbowe kumjulisha na tukakubaliana kupanga muda wa kuwasikiliza.
11. Kabla ya kuanza kuwasikiliza, msimamo wangu ulikuwa ni kumtaka Lowassa kwanza atangaze
kuhama chama, aweke wazi ni chama gani anaenda na ajisafishe juu ya tuhuma zake
12.Tangu akatwe jina, Lowassa hakutangaza kujitoa CCM na wala hakujisafisha na tuhuma zake, kitu
kilichonifanye nitofautiane naye.
13. Niliwauliza wanachadema wenzangu kuwa Lowassa anakuja kama Mtaji au Mzigo?
14. Swala sio urais kama watu wanavyozusha, mimi nilikuwa nataka mgombea mwenye uwezo na sifa
ambaye ataweza kuitoa CCM. Sikuwa na tamaa ya urais kama watu wanavyosema
15. Tangu Gwajima atupe taarifa za ujio wa Lowassa, Swali langu la Lowasssa kuwa Mtaji au mzigo
halikuwahi kujibiwa.
16. Nilitaka kujua ni mtaji gani lowassa atakuja nao na ni viongozi gan atakuja nao.
17. Nilijibiwa kuwa anakuja na wabunge 50 wa CCM, wenyeviti 22 wa mikoa na wenyeviti 80 wa
wilaya.
18.Baada ya ahadi hiyo, nilitaka sasa nipewe majina ya hawa watu lakini mpaka tarehe 25 july
sikupewa hayo majina
19. Wenzangu waliniambia kuwa tarehe 27 niitishe kikao cha dharura ila niligoma kwa sababu nilikuwa
sijapewa haya majina
20. Ndani ya kikao hicho, tulianza kwa mabishano makali kati yangu na Mbowe, Lissu na Gwajima,
viongozi wenzangu ni shahidi na mungu anajua. Msimamo wangu ulikuwa ni uleule kujua mchango wa
Lowassa
21. Kikao kile kikavunjika, baadae tukaingia kamati kuu lakini bado msimamo wangu ulikuwa ni uleule.
Baadae nikaandika barua ya kujiuzulu.
22.Profesa Safari aliichana ile barua.
23.Cha kusikitisha ni kuwa Kesho yake picha zikaanza kusambaa mtandaoni zikimuonyesha la lowassa
japo viongozi wangu walizikana zile picha. Kibaya ni kuwa viongozi waliuficha ukweli
24. Kesho yake niliandika tena barua rasmi ya kujiuzulu.
25. Baada ya pale zikaanza propaganda za uongo zikimuhusisha hadi mke wangu eti kanizuia.
26. Naomba watanzania wajue kuwa mke wangu hakuwahi kunizuia kwa lolote, lkn hata angefanya hivyo
sio mbaya maana hata yeye ni mwanaharakati mwenye uchungu na nchi hii.
27. Mke wangu aliwahi hadi kuumia wakati akipigania ukombozi wa nchi hii.....Lakini sio mbaya, familia
yangu imezoea propaganda.
28. Kikubwa katika harakati ni credibility ambayo lazima uilinde na mimi sitaki jina langu liharibiwe na
ni haki yangu.
29. Maslah mapana ya taifa ndiyo yaliyotufikisha hapa na sio maslahi binafsi.
30.Lowassa na wapambe wake ni waongo maana hakuna hata kipengele kimoja walichokitekeleza.
31. Tulitaka hao wabunge 50 waje kwanza kabla ya mchato wa uteuzi ccm
32. Napinga kuchukua makapi ya CCM kuyaita MTAJI.
33.Mtu kama Sumaye ni FISADI na nilikuwa siongei naye
34. Sumaye aliwahi kusema CCM wakimchagua Lowassa atahama chama. Leo Lowassa kawaje msafi??
35. Tulitaka Mtaji toka kwa Lowassa na sio MAKAPI
36. Wenyeviti walioletwa na Lowassa ni MZIGO na namjua vizuri. Akithubutu kunijibu ntamwaga UOZO
wake wote
37.Nani asiyejua Guninita pia ni mzigo??
38: Nawataka viongozi wangu wanijibu ni mtaji upi walioupata toka kwa Lowassa.
39. Mimi ni Padri Mstaafu, sipendi siasa za uongo.
39. Ukisema unataka kuiondoa CCM ni lazima ujikumbushe misingi ya CHADEMA ambayo ilikuwa ni
uadilifu. Leo chadema hii ina Uadilifu gani??
40. Namshangaa sana Lowassa eti kusimama mbele ya watu akijinasibu kuwa ni msafi.....kwamba
mwenye ushahidi aende Mahakamani. Ni dhambi kupotosha watu.
41. CCM hawana ujasiri, ni waoga na ndiyo maana wamewalea watu kama akina Lowassa
42. Ukitoa kinyesi chooni na kukipeleka Chumbani maana yake hata chumba chako ni CHOO na
kitakuwa kinanuka zaidi kulicho choo cha kawaida
43.Mimi nilikuwepo wakati sakata la Richmond likijadiliwa.Mimi nina ugomvi wa muda mrefu na
Lowassa.
44. Mwaka 2010 mimi nilimtaka Lowassa atangaze Richmond ni ya nani.
45. Leo tena namtaka Lowassa namtaka Lowassa atoke hadharani atangaze Richmond ni ya nani.
Unaposema ni ya mkubwa, atuambie mkubwa gani
46. Ukitaka kuijua Richmond rejea Ripoti ya Mwakyembe. Nampongeza Mwakyembe na Sitta kujitokeza
hadharan kuusema ukweli.
47. Siku moja kabla ya ripoti kusomwa, nililetewa Rushwa ya milioni 500 ili tukaupindishe ukweli
bungeni lakini nilikataa
48. Ripoti ya mwakyembe iliamua mambo mawili, moja; Lowassa ajipime au bunge lijadili na lichukue
ripoti. Lowassa kuona hivyo akaamua kukimbilia kujiuzulu kukwepa aibu ya kung'olewa na bunge
49: Lowassa haaminiki, ni muongo na hastahili kuwa Rais wa nchi....
50. Lowassa ni FISADI na kama mimi ni muongo ajitokeze hadharani akanushe
51. Anasema Lowassa ataleta maji, mbona jimbo lake la Monduli halina Maji???
52. Mnasema Lowassa kaanzisha shule za kata, iv mjua msingi wa shule za kata? waandishi rudini
shule mkajifunze upya.
53.Nilifanikiwa kuijenga Chadema na ikawa tumaini jipya la watanzania.....Vijana wangu wa Chadema,
naomba niwe mkweli propaganda imekivamia chama.
54. Inasikitisha kuona CHADEMA inajaza mabasi pale jangwani badala ya watu.....alafu mnawadanganya
watu eti ni MAFURIKO
55. CHADEMA ya kipindi changu ilikuwa inakemea Rushwa. Niambien leo chadema watasema nini
kwenye majukwaa?
56. Mnaomtetea Lowassa na nyie jitokezen hadharani...mimi nasema kwa sababu nina ushahidi na sio
lazima ushahidi huu niupeleke mahakamani.
57. Wenye uwezo wa kumpeleka Lowassa Mahakamani ni Serikali, na mwakyembe alisema juzi kuwa
kesi ya jinai haina kikomo, mtu anaweza kushitakiwa muda wowote
58. Sitaki kuingila swala la Babu Seya, lakini waliolawitiwa ni watoto waliokuwa chini ya umri. kwa nini
haki yao ipotee?
59. Rais hana mamlaka ya kumtoa Babu Seya. Lowassa asiwadanganye.
60. Kuhusu swala la Masheikh, Sumaye ndiye aliyeamuru mapolisi wavamie misikiti wakiwa na
mbwa......Watanzania msikubali kudanganywa. hizo ni propaganda za wasaka urais
61. Masikubali Rais Muongo na mimi naapa ntapiga kelele kila kona kumpinga Lowassa.
62.Lowassa alipokuwa waziri mkuu, matatizo yanayotokea leo hayakuwepo? mapigano ya wakulima na
wafugaji hayakuwepo?
63. Lowassa akiwa waziri mkuu alisababisha migogoro mizito sana kati ya monduli na karatu. Rais wa
aina hii wa nini?
64. Naomba nisiongee mengi kwa sababu ntakosa ya kusema siku nyingine.....Nawataka Lowassa na
Sumaye wajitokeze kunijibu.
65. Siku nyingine ntakuja kuongelea kuhusu hisa za Lowassa kwenye makampuni
66. Nahitimisha kwa kusema kuwa Nimestaafu siasa na sina chama lakini nina nchi, hivyo ntaendelea
kuwatumikia watanzania kwa jinsi mungu alivyonipa vipawa
67. Narudia tena, Sina chama na sitajiunga na chama chochote.
No comments:
Post a Comment