Menu

Sunday, September 6, 2015

*RAIS KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA MATANGAZO YA UTALII WA TANZANIA KIMATAIFA

 Baadhi ya vijana wa Kimasai maarufu kama Morani wakicheza ngoma ya kimasai ijulikanayo kama Laleyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya matangazo ya Utalii wa Tanzania kwenye vituo vya CNN na BBC uliofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mwanaye Khalfan Jakaya Kikwete pasi ya kudumu ya kuingia katika mbuga za wanyama ili kumtia moyo wa kupenda kutembelea mbuga hizo na kujenga tabia ya kuthamini uhifadhi wa maliasili ya taifa.Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu mbaye awali alimkabidhi Rais Pasi hiyo na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Adelhelm Meru.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Lazaro Nyalandu akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pasi maalum ya kudumu ya kuingia bure katika mbuga za wanyama kwa kutambua mchango wake ambnapo aliboresha sana huduma katika mbuga za wanyama na uhifadhi ikiwemo kuwarudisha faru kutoka Afrika ya kusini na kuboresha njia za mbugani kwa kipindi cha miaka kumi.
 Waziri wa maliasili na utalii  Mhe.Lazaro Nyalandu akimabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete picha ya kumbukumbu wakati Rais alipokuwa katika moja ya safari zake za utalii wa ndani katika mbuga ya Serengeti wakati wa likizo yake.Wanne kulia nia Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Adelhelm Meru,Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Bwana Alan Kijazi, na kulia ni kaimu Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) Bi Devotha Mdachi.
 Rais Kikwete, akipokea zawadi ya Kinyago
 Meza kuu
Picha na Fredy Maro

No comments:

Post a Comment