Menu

Tuesday, September 1, 2015

*SUCCOS KUANZISHA MIRADI YENYE LENGO LA KULETA AMANI NCHINI TANZANIA

Na Jenikisa Ndile -MAELEZO
Taasisi ya Succos Dar es salaam Foundation imeanzisha miradi iliobeba ujumbe wa kudumisha amani, upendo na umoja nchini yenye lengo la kuwasaidia wahitaji mbalimbali ili kuondokana na umasikini nchini. 

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Meneja Mradi Deogratius Paso amesema kuwa kupitia miradi hiyo itaendesha semina mbalimbali ambazo zitasaidia kudumisha amani na kupunguza umasikini nchini hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

 “Tumelenga mambo mbalimbali ambayo yatakua chachu ya kuendeleza amani nchini na kujikwamua na umasikini nchini ambapo taasisi yetu inatambua kuwa mdau wetu mkubwa ni Serikari ya Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania na kupitia serikari za mitaa itatusaidia kuwatambua wahitaji” alisema Deogratius.

Deogratius alisema kuwa taasisi yake imelenga kuandaa tamasha la michezo lenye lengo la kujumuika na kushirikiana kwa umoja, kujenga uwezo wa kuwapa elimu waitaji mbalimbali na kupunguza umasikini kupitia ujasiliamali.

Kupitia ujasiliamali huo, kutakuwa na miradi mbalimbali ambayo itakuwa endelevu kwa kuwahamasisha vijana kushiriki katika Mkuu wa mwaka huu wa kuwachagua Rais, Wabunge na Madiwani na hatimaye kupata viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano itakayopewa ridhaa na wananchi wenyewe.

No comments:

Post a Comment