Menu

Saturday, September 5, 2015

*UZINDUZI WA JENGO JIPYA LA MAGONJWA YA MOYO

 Waziri wa Afya, Seif Rashid (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick (kushoto) na mkuu wa kitengo, kwa pamoja wakikata utepe kuzindua Jengo jipya la magonjwa ya moyo, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo
 Waziri wa Afya, Seif Rashid, akipokea zawadi 
 Waziri wa Afya Seif Rashid akifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la uzinduzi wa Jengo hilo jipya la Magonjwa ya Moyo lililopo Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam leo. Waziri Seif alizindua Jengo hilo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete.
 Waziri wakivishwa vazi rasmi kwa ajili ya kuingia katika Wodi za wagonjwa wa Moyo waliokwisha fanyiwa upasuaji.
 Waziri Seif, akimsalimia mgonjwa aliyekwishafanyiwa upasuaji, Merikiory Kimwai,
 Waziri Seif, akimsalimia mtoto, Lilian Mwalingo (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Said Mecky Sadick
 Wauguzi wakimsaidia mtoto, Lilian Mwalingo, ambaye ni mmoja kati ya watoto wenye ugonjwa wa moyo wanaotibiwa katika jengo hilo jipya la ugonjwa wa moyo, baada ya uzinduzi huo.
 Waziri wa Afya, Seif Rashid (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, na baadhi ya viongozi wa Taasisi hiyo, wakimsalimia mtoto, Tito Thomas katika wodi ya Moyo.
 Waziri wa Afya, akisikiliza maelezo kuhusu mashine za kufanyia upasuaji wa moyo, kutoka kwa Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Tulizo Shem. 
 Burudani....
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo
Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi.

No comments:

Post a Comment