Menu

Tuesday, September 8, 2015

*ZOEZI LA KUGAWA CHAKULA KWA WAKIMBIZI LAENDELEA KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI YA NYARUGUSU KASULU MKOANI KIGOMA

 Wakimbizi kutoka nchini Burundi  walio katika kambi ya Nyarugusu wakiwa wamebeba Viroba vya Unga wa Mahindi jana, muda mfupi baada ya kugawiwa chakula hicho na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP), lililoweka kituo chake katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
 Byesige Josephat (anaye mimina mafuta) na Hezron Mtangirwa (kushoto), wakimbizi kutoka Burundi waliohifadhiwa kambi ya Nyarugusu wakipima mafuta ili waweze kuyagawa kwa wakimbizi wenzao jana, 
 Kinamama wakimbizi toka Burundi wakipata mgao wao wa unga
 Mkimbizi Irene Ntibelenda (katikati) akiwa pamoja na ndugu yake Sengiyu Mvajeme (kulia) baada ya kupokea mgao wa chakula 
 Josef Ntukugurya akifunga Viroba vya unga wa mahindi jana baada ya kupokea mgao 
Sehemu ya shehena ya chakula. PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment