Menu

Monday, September 7, 2015

*ZOEZI LA KUWAPOKEA WAKIMBIZI KUTOKA BURUNDI LAENDELEA KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI NYARUGUSU KIGOMA

Mtoto Jamine Nibetanga (14), kutoka nchini Burundi akiandaa chakula katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka nchini Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Karago na Mtendeli.
Baadhi ya wakimbizi kutoka nchini Burundi, Jacqueline Elulu (mwenye mtoto), na wenzake wakisubiri kupat ahuduma ya afya katika kituo cha Red Cross kinachotoa huduma za afya kwa wakimbizi walio katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Shirika la Red Cross ni moja ya wadau wanaoshirikiana na Serikali kutoa huduma za afya katika kambi ya Nyarugusu.
Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi wanaohifadhiwa katika Kambi ya Nyarugusu wakicheza mpira 
Mkuu wa Kambi yaWakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Fredrick Nisajile akiongea na wakimbizi walio katika mpango wa kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Mtendeli na Karago. Wakimbizi hao waliopokelewa kutoka nchini Burundi hivi karibuni kwa sasa wanahifadhiwa kwa muda katika kambi ya Nyarugusu.
Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi wakichota maji  katika moja ya vituo vya maji vilivyowekwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu B 
Mtagura akiandaa mihogo ya kuwauzia wakimbizi wenzake wanaoishi katika Kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Ntirampeba Acquelina akianika Mihogo ambayo huwauzia wenzake katika kambi hiyo ya Nyarugusu B 
Baadhi ya wakimbizi wakiwa katika harakati za kujitafutia kipato kwa kuuza mbogaboga kwa wenzao.
Mkimbizi Haverimana Ejide (kulia) na mkewe Kugimana Evona pamoja na watoto wao wakipata chakula cha mchana katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B.

(PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

No comments:

Post a Comment