Habari za Punde

*UJUMBE WA UBALOZI WA CHINA NCHINI WAMTEMBELEA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

 Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lu Youqing , akisaini kitabu cha wageni mara baadaya kuwasili katika Ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia), ofisini kwake alipowasili Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ziara fupi.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini, Lu Youqin akizungumza katika kikao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Charles Kitwanga (wa pili upande wa kushoto).  Katika kikao hicho kilichofanyika Wizara hapo, viongozi hawa walijadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Serikali ya China na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia), akizungumza na ujumbe wa Ubalozi wa China  nchini Tanzania, ulioongozwa na Balozi LuYouqing, (hawapo pichani), katika mkutano uliojumuisha pande hizo mbili kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali ya Watu wa China na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wa nne kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania, ulioongozwa na Balozi Lu Youqing (watatu kutoka kulia). Ujumbe huo ulitembelea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kujadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.