Habari za Punde

*YANGA SASA KUSUBIRI MSHINDI WA PILI WA KUNDI A, BAADA YA KUICHAPA MTIBWA SUGAR MAPINDUZI CUP


Wachezaji wa Yanga, Paul Nonga na Mbuyu Twite, wakimpongeza Malimi Busungu, aada ya kufunga bao la pili katika mchezo wa hatua ya makundi kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea mjini Zzanzibar. Katika mchezo huo Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtiwa Sugar. Katika mchezo wa awali kati ya Azam Fc na Mafunzo, Mafunzo waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuwafanya Azam kufungasha virago katika michuano hiyo.
*******************************************
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
TIMU ya Yanga SC usiku huu imefikisha jumla ya Pointi Saba katika kundi B baada ya kuinyuka Mtibwa Sugar kwa mabao 2-1 kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayoendelea mjini, Zanzibar.

Yanga SC imeshinda mechi mbili na kutoa sare moja, hivyo kuwa kileleni mwa Kundi B ikifuatiwa na Mtibwa iliyomaliza na pointi nne, Mafunzo pointi tatu, wakati Azam FC waliovuna pointi mbili wakishika mkia na kuaga Mashindano hayo.

Yanga SC sasa itacheza na mshindi wa pili wa Kundi A katika Nusu Fainali, wakati Mtibwa Sugar itacheza na mshindi wa pili wa kundi hilo.

Mtibwa Sugar walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa kiungo wake, Shizza Kichuya aliyemalizia pasi ya mshambuliaji anayecheza kwa mkopo timu hiyo ya Manungu kutoka Yanga SC, Hussein Javu.

Yanga SC walifanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa kiungo wake mpya kutoka Niger, Boubacar Issoufou, katika dakika ya 42, kwa mpira wa adhabu baada ya Donald Ngoma kuchezewa faulo na beki wa Mtibwa Salum Mbonde karibu kabisa na eneo la hatari kutoka pembeni kulia nje kidogo ya boksi.

Alikuwa ni mshambuliaji Malimi Busungu aliyetokea benchi, kuchukua nafasi ya Amis Tambwe, ambaye alipachika bao la pili na la ushindi katika dakika ya 81 akimalizia krosi nzuri ya winga Simon Msuva.

Kiungo wa Mtibwa Sugar, Henry Joseph aliyetokea benchi kipindi cha pili, alitolewa kwa kadi nyekundu dakika za mwishoni baada ya kumchezea rafu Simon Msuva kabla ya kumchezea rafu pia Salum Telela.

Mechi za makundi zinatarajiwa kuhitimishwa kesho kwa michezo ya Kundi A, kati ya URA na Jamhuri jioni na Simba SC na JKU usiku.
Hadi sasa, Simba SC inaongoza Kundi A kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na URA na JKU zenye pointi tatu kila moja.

KiIKOSI CHA YANGA SC: Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondan/Pato Ngonyani dk89, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko/Salum Telela dk74, Donald Ngoma/Paul Nonga dk65, Amisi Tambwe/Malimi Busungu dk56 na Boubacar Issoufou/Boubacar Issoufou dk71.

KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR: Said Mohammed, Ally Shomary, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Andrew Vincent/Dickson Daud dk10, Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Shizza Kichuya, Muzamil Yassin, Hussein Javu/Said Bahanuzi dk63, Ibrahim Rajab ‘Jeba’/Henry Joseph dk76 na Vincent Barnabas/Mohamed Ibrahim dk56. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.