Gari lenye namba za usajili T 709 AYW likiwa limeegeshwa kwenye kidaraja cha kuvushia magari kuingia kwenye kivuko, gari hilo kunusurika kutumbukia Baharini kwa kutofuata sheria za vivuko kwa kujaza mzigo mkubwa wa Barafu ambazo haikuweza kufahamika mara moja zilikuwa na uzito gani na zilikuwa zikipeleka wapi.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 11: 25 alasiri wakati gari hilo likiingia katika kivuko cha MV Lami na kunasa kwenye mlango wa kivuko hicho kutokana na gari hilo kuzidisha uzito wa mzigo mkubwa uliokuwa ndani yake na kusababisha kunasa katika mlango huo wa MV Lami.
Baada ya tukio hilo ilibidi kushushwa mabarafu yote na kisha ari hilo hilo likavutwa na gari jingine ili kulinusuru kutotumbukia majini na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Juhudi za kulinusuru gari hilo zikiendelea....
Gari hilo likisukumwa...
No comments:
Post a Comment